Simon Kimbangu
Simon Kimbangu (12 Septemba 1887 - 12 Oktoba 1951) alikuwa mwinjilisti wa Kibaptisti Kongo ya Kibelgiji aliyeonekana kuwa na karama ya uponyaji.
Watu wengi walimwendea kutafuta nafuu wakasikia mahubiri yake, lakini serikali ya kikoloni ya Ubelgiji iliogopa mikutano mikubwa ya Waafrika bila usimamizi wa Wazungu au machifu.
Hivyo Kimbangu akaagizwa na wamisionari kwa amri ya serikali aache mahubiri na uponyaji lakini hakuweza kutii.
Wabelgiji wakamkamata wakamfunga gerezani miaka mingi mpaka kifo. Kabla hajafa alimuomba sista aliyemuuguza ambatize Kikatoliki akakubaliwa kwa kupewa ubatizo wa sharti.
Wafuasi wake wakamwamini kuwa nabii wa Mungu, wengine walisema ndiye Yesu aliyerudi, wakatoka katika uongozi wa wamisionari walionyamaza mbele ya tendo la serikali la kumfunga Kimbangu bila kosa.
Kati ya wafuasi wake limetokea "Kanisa la Kristo kwa Mtume wake Simon Kimbangu" ambalo leo lina waumini milioni kadhaa katika nchi kadhaa.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Bethel University site Ilihifadhiwa 24 Julai 2010 kwenye Wayback Machine.
- Encyclopædia Britannica
- Simonkimbangu.org Ilihifadhiwa 11 Mei 2016 kwenye Wayback Machine.
- kimbangudiscoveries.com Ilihifadhiwa 18 Januari 2019 kwenye Wayback Machine.
- Dictionary of African Christian Biography: Simon Kimbangu, article reprinted from An African Biographical Dictionary, copyright © 1994, edited by Norbert C. Brockman, Santa Barbara, California.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |