Sildenafil

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kidonge cha Viagra toka kampuni ya Pfizer

Sildenafil (huuzwa kwa jina la Viagra kati ya majina mengine) ni dawa inayotumika kutibu tatizo la kusimama kwa uume na shinikizo la damu la mshipa mkubwa mapafuni.[1]

Ufanisi wake katika kutibu tatizo kama hilo kwa wanawake haujathibitishwa kikamilifu ingawa zipo kampuni zinazodai kuwa na dawa hii.[1]

Madhara ya kawaida ya dawa hii yanajumuisha maumivu ya kichwa na kiungulia. Tahadhari inatolewa kwa wale ambao wana ugonjwa wa moyo. Madhara makubwa yanajumuisha kusimama kwa uume kwa muda mrefu, ambapo huweza kusababisha uharibifu wa uume.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wanasayansi wa kampuni ya Pfizer Andrew Bell, David Brown na Nicholas Terrett awali waligundua sildenafil kama matibabu kwa matatizo mbalimbali ya mishipa ya moyo.[2][3]

Tangu kuanza kutumika kwake mwaka 1998, sildenafil imekuwa matibabu ya kawaida kwa matatizo ya kusimama kwa uume; washindani wake wakubwa ni dawa za tadalafil (jina la kibiashara Cialis) na vardenafil (Levitra).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Sildenafil Citrate". The American Society of Health-System Pharmacists. Iliwekwa mnamo 1 Desemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Patent US5250534 - Pyrazolopyrimidinone antianginal agents - Google Patents".
  3. Boolell, M; Allen, MJ; Ballard, SA; Gepi-Attee, S; Muirhead, GJ; Naylor, AM; Osterloh, IH; Gingell, C (Juni 1996). "Sildenafil: an Orally Active Type 5 Cyclic GMP-Specific Phosphodiesterase Inhibitor for the Treatment of Penile Erectile Dysfunction". International Journal of Impotence Research. 8 (2): 47–52. PMID 8858389.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sildenafil kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.