Nenda kwa yaliyomo

Kiungulia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kiungulia (kwa Kiingereza heartburn) ni hali ya kusikia maumivu makali katika koo la chakula.

Maumivu hayo yanatokana na kupanda kwa asidi iliyomo tumboni (asidi haidrokloriki = HCl) inayofanya kazi ya kuua vijidudu vinavyoingia tumboni kwa njia ya chakula na maji.

Mara nyingi kiungulia kikatokea baada ya tumbo kujaa gesi.

Kiungulia kinaweza kuwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kula kwa pupa au kupita kiasi, matumizi ya dawa za kulevya, ujauzito, tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo n.k.

Namna ya kuzuia kiungulia

[hariri | hariri chanzo]

Kiungulia kinaweza kuzuiwa kwa namna mbalimbali. Zifuatazo ni baadhi ya njia za kuzuia kiungulia:

  • Epuka kulala mara tu badaa ya kula chakula.
  • Epuka kula kupita kiasi.
  • Epuka kula vitu kama maharagwe, mboga za sukuma n.k.
  • Epuka vinywaji vyenye asidi kwa wingi, mfano: soda n.k.
  • Epuka matumizi ya dawa za kulevya.
  • Tumia mto pindi ulalapo

Tiba ya kiungulia inaweza kuwa ni ya asili au ya hospitali. Hivyo mtu anayesumbuliwa na kiungulia anaweza kutumia:

  1. Dawa za asili kama juisi ya tofaa au ya tangawizi.
  2. Dawa za hospitali kama Omeprazole ambayo japo huchukua muda kiasi lakini inakuwa na matokeo bora zaidi.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiungulia kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.