Seduce Me

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Seduce Me”
“Seduce Me” cover
Single ya Ali Kiba
Imetolewa 25 Agosti 2017
Muundo Upakuzi mtandaoni
Imerekodiwa 2017
Aina Bongo Flava
Urefu 3:21
Studio Combination Sound
Mtunzi Ali Kiba
Mtayarishaji Man Walter
Mwenendo wa single za Ali Kiba
"Aje Remix"
(2017)
"Seduce Me"
(2017)
Video ya muziki
"Seduce Me" katika YouTube

"Seduce Me" ni jina la wimbo wa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Ali Kiba. Wimbo umetayarishwa na Man Walter kupitia studio za Combination Sound za jijini Dar es Salaam. Ukiwa kama sehemu ya usambazaji na kampuni ya "Sony Music Entertainment Africa" ya tawi la Afrika Kusini. Huu ni wimbo wa kwanza wa Ali Kiba kupata watazamaji milioni moja katika Youtube ndani ya masaa 38 tu tangu kutolewa kwake.[1] [2]

Wimbo huu umezua maneno mengi hasa baada ya kutoka tu, Diamond Platnumz akaweka bandiko katika ukurasa wake wa Instagram la mtu mmoja anacheka bila maoni yoyote katika bandiko hilo. Usiku wake, Diamond akatoa wimbo wake mpya akiwa na vijana wake wa Wasafi Records - Zilipendwa. Kumekuwa na malumbano ya hapa na pale kwa kufuatia visa vilivyokuwa vikiendelea hivi karibuni kwa kitendo cha Diamond kumuimba Ali Kiba kwa kejeli katika wimbo aliourudia wa Fid Q Fresh na hatimaye Kiba nae kujibu kwa kejeli na haijapita siku nyingi Kiba akatoa wimbo huu kwa kuonesha majigambo yake ya ufalme wa Bongo Flava.

Mapokeo na maoni mbalimbali[hariri | hariri chanzo]

Kumekuwa na dhana nyingi zinazotolewa na wadau mbalimbali wa muziki huenda majigambo na tambo zilizotolewa hivi karibu ndizo hasa zilizopelekea kusukuma wimbo wa "Seduce Me" kufikia kiwango cha watazamaji milioni moja ndani ya masaa 24. Wengine wanahisi huenda kitendo cha Diamond kuposti picha ya jamaa anacheka, ndiyo hasa iliyopelekea wengi kutaka kuuona wimbo uliotoka wa Ali Kiba hadi Diamond aukosoe au kuweka kicheko kile. Wimbo umependwa na wasanii mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Professor Jay aliweka bandiko la kumsifu Ali Kiba katika ukurasa wake wa Instagram - akionesha hisia zake kwa wimbo huo.[3] Vilevile mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania mwenye makazi yake kwa sasa nchini Kenya Bi. Christina Shusho amefurahishwa na uimbaji wa Kiba na kutia mzaha kuwa "Leo unaweza kuta mtu kaitwa kanisani aongoze wimbo wa sifa halafu akalianzisha Seduce Me….eeh jamani Kiba we noma.". Vilevile amesifia maudhui na picha za video zina heshima kiasi unaweza kuangalia na rika zote.[4] Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Mawawikili Tanganyika Mh. Tundu Lissu nae alionekana kutoa maoni yake juu ya wimbo huu wa "Seduce Me" katika ukurasa wake wa Twitter aliandika: "Hakuna kitu kibaya kama wanaume sita kuvaa mawigi na kupambana na mtu mmoja".[5] Jambo hili yalitolewa mapovu mengi hasa baada ya kuona mtu mkubwa kama huyu akiingilia mambo ya muziki wa vijana. Wengi wao walionekana kumuunga mkono kwa kuonesha hisia zake. Baadaye ikaja kugundulika kuwa ile akaunti si ya Tundu Lissu, lakini ni miongoni mwa akaunti ambayo inafanya kazi kila wakati kuliko hata ile ya Lissu mwenyewe.[6] Wasanii wengine mbalimbali walionekana kuufurahia wimbo kwa kuweka video kadhaa zinazoonesha kuupiga wimbo huu kwa nyuma.[7]

Video ya muziki[hariri | hariri chanzo]

Video inaanza kwa kuonesha mtu na mpenzi wake wakiwa wametoka kufanya uhalifu mahali fulani na kuiba mapesa ya maana. Baadaye wanaonekana chumbani wakijirusha kwa mafanikio walioyapata katika tukio walilotenda. Mwisho inaonekana Ali Kiba kuingizwa mjini na yule mwanamama aliyeshiriki nae katika kuiba pesa zile. Ni video ya kawaida, lakini ina ubunifu mkubwa.


Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Kigezo:Alikiba