Nenda kwa yaliyomo

Aje

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Aje Remix)
“Aje”
“Aje” cover
Kava la Aje
Single ya Ali Kiba
Imetolewa 2016
Muundo Upakuzi mtandaoni
Imerekodiwa 2016
Aina Pop, Bongo Flava
Urefu 3:43
Studio Sony Music Entertainment
Mtayarishaji Abby Daddy
Mwenendo wa single za Ali Kiba
"Lupela"
(2016)
"Aje"
(2016)
"Seduce Me"
(2017)
Kava lingine la Aje
Kava la Aje Remix
Kava la Aje Remix

"Aje" ni jina la wimbo uliotoka 2016 wa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Ali Kiba. Wimbo umetayarishwa na Abby Daddy ukiwa wimbo wa pili kufanya pamoja nae baada ya ule wa Chekecha Cheketua. Awali walifanya nyimbo kadhaa lakini hazikufuzu kuingia katika orodha ya nyimbo rasmi za Kiba. Aje ni wimbo wa kwanza wa Ali Kiba kusambazwa na Sony Music Entertainment kwa ushirikiano na lebo mwenza ya Kiba Rockstar4000 ambayo Kiba ana hisa.

Aje ni mchanganyiko wa Afro-pop na Bongo Flava iliyo na hisia kali kwa msikilizaji. Kiba ameonesha ufundi wa hali ya juu si tu katika sauti, bali pia katika utengenezwaji wa video yake. Video imeongozwa na Meji Alabi kutoka nchini Nigeria - na ndiye huyuhuyu aliyeongoza video ya Chekecha Cheketua. Mnamo tarehe 16 Februari, 2017, Kiba akatoa remix ya Aje iliyomshirikisha rapa wa Kinigeria M.I. Video imeongozwa na Meji Alabi lakini kwa bahati mbaya M.I. hajaonekana kwenye video. Ila tu inasifika kwa kutumia maneno ya Kiswahili kwa msanii huyo wa Nigeria - kitu ambacho kilileta hamasa kubwa kwa wazungumzaji wa Kiswahili.[1] Kingine remix ya Aje inasifika kwa Ali kufanya ubobishi mwishoni mwa video. Mambo ambayo hakufanya hapo awali katika video zake.[2]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Aje Niaje.com Archived 13 Mei 2016 at the Wayback Machine. New Music: Alikiba Drops ‘Aje’ Featuring Nigerian Rapper M.I - Niaje.com
  2. Aje360Nobs.com Archived 12 Machi 2017 at the Wayback Machine. Tanzanian Award winning recording artist, singer-songwriter Ali Saleh Kiba, better known by his stage name Ali Kiba, is back with the visuals to his smash hit single “Aje (Remix)” which he features Nigerian Rap Star – M.I Abaga.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]