Nenda kwa yaliyomo

Nagharamia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Nagharamia”
“Nagharamia” cover
Kava ya Nagharamia
Single ya Ali Kiba akiwa na Christian Bella
Imetolewa 19 Disemba, 2015
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2015
Aina Pop, Bongo Flava, Bella Flava, Muziki wa dansi
Urefu 3:59
Studio RockStar4000
Mtunzi Ali Kiba
Christian Bella
Mtayarishaji Abby Daddy
Mwenendo wa single za Ali Kiba akiwa na Christian Bella
"Chekecha Cheketua"
(2015)
"Nagharamia"
(2015)
"Lupela"
2016

"Nagharamia" ni jina la wimbo uliotoka 19 Disemba 2015 wa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Ali Kiba akiwa na mfalme wa masauti Christian Bella. Wimbo umetayarishwa na Abby Daddy ukiwa wimbo wa tatu kutolewa tangu kusimama kutoa kazi za kujitegemea miaka mitatu iliyopita. Vilevile huhesabiwa kama wimbo wa kwanza kumshirikisha mtu tangu kurudi kwake katika muziki mazima. Bella kafanya balaa zito humu kupita kiasi. Ujibizanaji baina ya waimbaji ni wa kipekee tangu Unanitega ya Noorah na Mwana FA na ya hivi karibuni iliyofanywa na Roma na Stamina Hivi Ama Vile. Video ya wimbo huu iliongozwa na Enos Olik kutoka Kenya na ndiye aliyekuja kuongoza video ya kucheza dansi la wimbo wa Sauti Sol wakiwa na Kiba Unconditionally Bae uliotoka Machi 10, 2016.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]