Mwana (wimbo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Mwana”
“Mwana” cover
Kava ya Mwana
Single ya Ali Kiba
Imetolewa 18 Disemba, 2014
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2010
Aina Pop, Bongo Flava
Urefu 3:54
Studio Combination Sound
Mtunzi Ali Kiba
Chix Vallo
Mtayarishaji Man Walter
Mwenendo wa single za Ali Kiba
Kibela - 2013 Mwana
2014
Chekecha Cheketua
2015

"Mwana" ni jina la wimbo uliotoka Disemba 18 2014 wa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Ali Kiba. Wimbo umetayarishwa na Man Walter ukiwa wimbo wa kwanza kutoka tangu kusimama kutoa kazi za kujitegemea miaka mitatu iliyopita.

Vilevile huhesabiwa kama wimbo wa kwanza kutolewa akiwa na ushirikiano na lebo ya Rockstar4000 na Rockstar Publishing - ambayo Kiba ana hisa. Video ya wimbo huu iliongozwa na Godfather Production kutoka Afrika Kusini. Hii ni video ya kwanza ya Kiba kupiga nchi za nje na ya kwanza kwa gharama kubwa tangu kurudi kwake katika muziki.

Kulingana na mtayarishaji wa wimbo huu Man Walter, anasema wimbo huu ulikaa studio bila kutolewa miaka minne. Hadi hapo aliporudi tena na kuanza kuchagua baadhi ya nyimbo kwa ajili ya ujio mpya. Msanii mwingine ni Mr. blue wimbo wake wa Nipende Kama Nilivyo umekaa miaka mitano, alisema Man Walter.[1]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Wimbo wa Kiba Mwana miaka minne studio Unajua muda ambao ‘Mwana’ ya Ali Kiba na Blue. Millard Ayo.com

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]