Fid Q

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Fid Q
Fid Q akionyesha kidole cha shahada - akiashiria wimbo wake wa "Chagua Moja".
Fid Q akionyesha kidole cha shahada - akiashiria wimbo wake wa "Chagua Moja".
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Jina la kisanii Fid Q
Nchi Tanzania
Alizaliwa 13 Agosti 1982
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Mwanamuziki
Ameshirikiana na Juma Nature
Professor Jay
Witness
Ngwair
Mr. Paul
Daz Baba
Langa Kileo
Black Rhino
T.I.D.
Adiri
Diamond Platnumz
Rayvanny
Fresh
Ala Sauti
Kampuni Bongo Records
Mj Records
Baucha Records

Farid Kubanda (amezaliwa tarehe 13 Agosti 1982, katika hospitali ya Bugando iliyopo jijini Mwanza) ni msanii wa hip hop na Bongo Flava kutoka nchini Tanzania.

Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Fid Q.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Fid Q, 2013

Shughuli za awali (kwa ufupi)[hariri | hariri chanzo]

Fid Q alianza shughuli za muziki mnamo miaka ya 1990. Fid Q alitoa kibao chake cha kwanza mwaka 2000 kiitwacho 'Huyu na Yule' ambacho hicho aliimba na msanii Mr Paul. Kibao hiki kilimpa heshima kubwa, kibao hicho kilirekodiwa katika studio za MJ records chini ya usimamizi wake Master Jay mwenyewe.

Kibao chake cha pili kutoka kiliitwa 'Binti Malkia' ambacho alimshirikisha Noorelly. Ilivyofika mnamo mwaka wa 2004 Fid Q alivunja ukimya wake kwa kibao chake mahili kilichokwenda kwa jina la "Fid Q.com", na kibao hicho alikifanya katika studi ya Baucha Records baada ya kuhama kwa MJ.

Kibao hicho kiliirudisha ile hiphop ya Tanzania katika ramani yake halisi na inasemekana hivyo kwasababu kipindi hicho ni kile ambacho wasaanii wengi wa muziki wa kufokafoka walikuwa wamejiingiza katika masuala ya uimbaji kwasababu kulikuwa na uvumi wa kwamba hip hop haikubaliki kwa watu wa Tanzania.

Fid anatajwa kuwa Ni miongoni mwa wasanii walioleta heshima ya hip hop Tanzania na Afrika mashariki na kibao chake kinachojulikana kama Mwanzamwanza kilifanya vizuri ambapo ndani yake kuna uandishi wa kipekee ambao umeenda tofaut na ule uliokuwa umezoeleka(masimulizi/mipasho)

Mara kadhaa amekuwa akitajwa kama mwanahip hop bora wa muda wote Tanzania na Afrika mashariki (na Felix Nyaumbu).

Ilipofika 26 Januari ya mwaka 2008, Fid Q alipakua kibao kiitwacho "Ni Hayo Tu" alichomshirikisha Prof. J na Langa. Kibao hicho kilibahatika kujinyakulia Tuzo ya Kili kikiwa kama kibao bora cha muziki wa hip hop kwa mwaka wa 2007-2008.

Fid Q ana albamu mbili kwenye soko la muziki. Albamu ya kwanza inaitwa inayoitwa "Vina Mwanzo Kati na Mwisho".[1] Mwishoni mwa mwaka 2009 alitoa albamu ya pili "PROPAGANDA", ambayo imepokelewa vizuri sana Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Mashabiki wa Hip Hop wanaichukulia PROPAGANDA kama ni albamu bora kabisa, yaani 'classic'. Hivi karibuni anategemea kutoa albamu yake ya tatu itakayokwenda kwa jina la "KitaaOLOJIA".

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fid Q kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.