Witness

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Witness
Jina la kuzaliwa Witness Fred Mwaijaga
Amezaliwa 15 Novemba 1982 (1982-11-15) (umri 36)
Asili yake Dar es Salaam, Tanzania
Aina ya muziki Hip hop, rap
Kazi yake Rapa
Ala Sauti
Ame/Wameshirikiana na Fid Q, Langa Kileo, Sarah Kaisi, Mr. Abel

Witness Fred Mwaijaga (anafahamika kwa jina lake la kisanii kama Witness "au" Bad Jiah; amezaliwa 15 Novemba 1982) ni msanii wa hip hop na rapa kutoka nchini Tanzania.

Anafahamika zaidi kwa kuwa mmoja kati ya washindi wa shindano la Coca Cola Pop Stars na mmoja wa waanzilishi wa kundi la muziki wa hip hop maarufu kama Wakilisha. Anavuma kwa baadhi ya vibao vyake kadhaa alivyofanya na kundi, pamoja na vya peke yake. Vibao hivyo ni pamoja na: Hoi, Kiswanglish, Kichekesho na Zero.

Witness, alisoma katika Shule ya Msingi ya Oysterbay ya jijini Dar es Salaam, vilevile Shule ya Sekondari ya Jitegemee ambapo ndipo alipomazia. Pia, alishafanya kazi na mashirika ya kimataifa kama vile Unicef na alikuwa akifanya mikutano inayohusiana na masuala ya vijana.

Pia, alishawahi kuwa mnenguaji wa ngoma za asili wa ISHI, shirika la maendeleo ya vijana Tanzania.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  • Witness katika Tanzania Directoty.info
Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Witness kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.