Samuel Wanjiru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rekodi za medali

Samuel Wanjiru
Men's Wanariadha
Anawakilisha nchi Bendera ya Kenya Kenya
Michezo ya Olimpiki
Dhahabu 2008 Beijing Marathon

Samuel Kamau Wanjiru (Nyahururu, 10 Novemba 1986 - 15 Mei 2011) alikuwa mwanariadha wa Kenya ambaye mbio zake maalumu zilikuwa mbio za masafa marefu akawa bingwa katika umri mdogo na kuvunja rekodi ya dunia ya nusu marathon alipokuwa na umri wa miaka 18. Mwaka 2007, alivunja rekodi ya kukimbia ya barabara ya kilomita 20 na kuboresha rekodi ya nusu marathon kwa zaidi ya sekunde ishirini.

Alihamia hadi marathoni kamili na alishinda katika Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka wa 2008 kwa muda ambao ulikuwa rekodi ya Olimpiki wa masaa 2:06:32 na kuwa Mkenya wa kwanza kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki katika marathon. Mwaka uliofuata, alishinda marathon zote mbili za London Marathon na Chicago Marathon, kwa kukimbia marathon ya kasi zaidi milele kurekodiwa katika nchi za Uingereza na Marekani.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Wanjiru alianza mbio akiwa na umri wa miaka 15. Mwaka wa 2002, alihamia Ujapani akajiunga na shule ya upili ya Sendai Ikuei Gakuen katika sehemu ya Sendai, ambapo alihitimu mwaka wa 2005. Kisha alijiunga na timu ya raidha ya Toyota Kyushu iliyokuwa inafunzwa na mshindi wa medali ya fedha katika mbio za marathon katika Olimpiki ya mwaka wa 1992, Koichi Morishita.

Muda bora wa Wanjiru katika mbio za mita 5,000 ni dakika 13:12.40, muda aliyouweka akiwa na umri wa miaka 17 mnamo Aprili 2004 mjini Hiroshima, Ujapani. Akiwa na umri wa miaka 18 tu, Wanjiru alivunja rekodi ya dunia ya nusu marathon mnamo 11 Septemba 2005 katika Nusu marathon ya Rotterdam kwa muda wa dakika 59:16 na akaivunja rasmi rekodi ya Paul Tergat nusu-marathon ya dakika 59:17. Hii ilitangulia mapema wiki mbili kwa kuboresha kwa rekodi ya vijana ya dunia ya mita 10,000 kwa karibu sekunde 23 katika IAAF Golden League Van Damme Memorial Race mnamo 26 Agosti. Rekodi yake ya dunia ya vijana ya dakika 26:41.75 ilikuwa nzuri sana kumpa nafasi ya tatu katika mbio hizo nyuma ya rekodi ya dunia ya Kenenisa Bekele ya dakika 26:17.53 na ya Boniface Kiprop ya dakika 26:39.77. Ilikuwa Kiprop ambaye alikuwa anashikilia rekodi ya dunia ya vijana (dakika 27:04.00) ambayo iliwekwa katika michuano hiyo mwaka uliyokuwa umepita.

2007-2008[hariri | hariri chanzo]

Kwa mara nyingine Wanjiru alichukuwa tena rekodi ya dunia ya nusu marathon, ambayo Haile Gebrselassie alikuwa amevunja mapema mwaka wa 2006, kwa dakika 58:53 mnamo 9 Februari 2007 katika marathon ya Ras Al Khaimah Nusu [8] na kuiboresha kwa muda wa dakika 58:33 mnamo 17 Machi 2007 katika City-Pier-City Loop katika mji mkuu wa Hague nchini Uholanzi. Huku akiiboresha rekodi yake ya kibinafsi pia alivunja rekodi ya dunia ya Haile Gebrselassie katika mbio za kilomita 20 kwa muda wa dakika 55:31, uboresho wa sekunde 17.

Wanjiru alikimbia marathon yake kamili ya kwanza katika marathon ya Fukuoka mnamo 2 Desemba 2007 na kuishinda mbio hiyo kwa njia ya kusisimua kwa rekodi ya kozi ya saa 2:06:39. Katika marathon ya London ya mwaka wa 2008, alimaliza katika nafasi ya pili na kuivunja 2:06 kwa mara ya kwanza. Katika Olimpiki ya mwaka wa 2008, Wanjiru alishinda medali ya dhahabu katika marathon katika muda wa rekodi ya Olimpiki ya saa 2:06:32 na kuvunja rekodi ya awali ya saa 2:09:21 iliyowekwa na Carlos Lopes wa Ureno katika Olimpiki ya mwaka wa 1984.

2009[hariri | hariri chanzo]

Katika Mitja Marató de Granollers ya 24, ambayo Wanjiru alishinda, alinukuliwa akisema, "katika muda wa miaka mitano inayokuja najihisi nina uwezo wa kukimbia mbio za marathon kwa muda chini ya masaa 2 ". Mwezi Aprili mwaka wa 2009, Wanjiru alishinda marathon ya London kwa muda wa masaa 2:05:10, rekodi mpya ya kibinafsi na pia rekodi mpya ya kozi. Alifurahishwa sana na fanikio lake na kusema kuwa alitumai kuvunja rekodi ya dunia ya Haile Gebrselassie baadaye. Katika Nusu Marathon ya Rotterdam, Wanjiru alikimbia kwa muda wa saa 1:01:08 mnamo 13 Septemba, mbio ambayo ilishindwa na Sammy Kitwara kwa muda wa dakika 58:58. ] Mnamo Oktoba mwaka wa 2009, Wanjiru alishinda Marathon ya Chicago kwa muda wa saa 2:05:41 na kuweka rekodi mpya ya kozi katika mji huo mkuu na muda wa kasi zaidi katika marathon milele kukimbiwa nchini Marekani. Ushindi wake katika miji mikuu ya London na Chicago yalimsaidia kufikia nafasi ya juu ya orodha kuu ya dunia katika Marathon mwaka wa 2009 na kumtuza jackpot ya dola 500,000 za Marekani.

Maisha ya Kibinafsi.[hariri | hariri chanzo]

Binamu wake Joseph Riri ni mwanariadha wa daraja ya dunia katika mbio za marathon, [16] na kakake mdogo Wanjiru, Simoni Njoroge pia ni mkimbiaji wa masafa marefu. Wanjiru alipewa mawaidha na Stephen Ndungu, mwanariadha wa mbio za marathon na mtengeneza kasi.

Wanjiru alikuwa mumewe Triza Wanjiru na walikuwa na watoto wawili. Hata hivyo, Wanjiru alikuwa mpenda anasa kupita na inasemekana alikuwa na wapenzi kadhaa. Kufuatia kuaga kwake, wanawake kadhaa walijitokeza wakidai urithi, wakiwemo Judy Wambui ambaye alikuwa mja mzito kupitia Wanjiru.

Wanjiru alituzwa tuzo la mwanaspoti wa mwaka anayeahadi sana nchini Kenya mwaka wa 2005.

Alishinda tuzo la mwanaspoti wa mwaka wa Kenya mwaka wa 2008.

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Katika usiku wa 15 Mei 2011, Wanjiru alifariki baada ya kuanguka kutoka juu ya nyumba yake katika mji wa Nyahururu. Kufuatia upelelezi kuhusu kifo chake, ilionekana kifo chake kilitokana na majeruhi baaada ya kuanguka. Wanjiru alitangazwa kwamba amekufa na madaktari katika hospitali iliyoko karibu na alikoishi.[1]

Katika mwezi wa Mei 2017, huku akitoa ushahidi mbele ya jopo maalum lililoumbwa kuchunguza kifo cha Wanjiru, mamake Hannah Wanjiru aliliambia jopo hilo katika korti la Milimani kuwa bila shaka lolote, aliamini mwanawe kauwawa na majambazi sita waliokuwa wakishirikiana na mkewe Wanjiru, Trizah Njeri.[2][3][4]

Ubora binafsi[hariri | hariri chanzo]

Samuel Wanjiru, akivunja rekodi ya ulimwengu mwaka wa 2007 katika Nusu Marathon ya Fortis City-Pier-City
Tukio Muda Tarehe Kikao chake
Mita5000 metres 13:12.40 29 Aprili 2005 Hiroshima
Mita 10,000 mita 26:41.75 † 26 Agosti 2005 Brussels
Kilomita 20 55:31 ‡ 17 Machi 2007 Den Tundu
Nusu Marathon 58:33 ‡ 17 Machi 2007 Den Tundu
Marathon 2:05:10 17 Aprili 2009 London

Taarifa yote iliyochukuliwa kutoka kwa IAAF .

Key: † = rekodi ya dunia kwa vijana, ‡ = rekodi ya Dunia

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Polisi motoni katika kesi ya kifo cha Samuel Wanjiru – Taifa Leo" (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-07-08. 
  2. "Samuel Wanjiru’s mum claims six strange men seen on night of his death". Nairobi News (kwa en-US). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-08. Iliwekwa mnamo 2020-07-08. 
  3. "Bingwa wa Olimpiki, Wanjiru, mahakamani". BBC News Swahili (kwa Kiswahili). Iliwekwa mnamo 2020-07-08. 
  4. "Marathon hero Wanjiru was 'murdered in bedroom'- Mother". Citizentv.co.ke (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-07-08. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Records
Alitanguliwa na
Kenya Paul Tergat
Men's Half Marathon World Record Holder
11 Septemba 2005 – 15 Januari 2006
Akafuatiwa na
Ethiopia Haile Gebrselassie
Alitanguliwa na
Ethiopia Haile Gebrselassie
Men's Half Marathon World Record Holder
9 Februari 2007 –
Akafuatiwa na
Incumbent
Alitanguliwa na
Ethiopia Haile Gebrselassie
Men's 20 kilometres World Record Holder
17 Machi 2007
Akafuatiwa na
Incumbent|}
Sporting positions
Alitanguliwa na
Kenya Robert Kipkoech Cheruiyot
Rotterdam Men's Half Marathon Winner
2005
Akafuatiwa na
Eritrea Zersenay Tadese
Alitanguliwa na
Ethiopia Haile Gebrselassie
Men's Half Marathon Best Year Performance
2007
Akafuatiwa na
shared between
Ethiopia Haile Gebrselassie &
Ethiopia Deriba Merga
etablerade