Rudewa
Kata ya Rudewa | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Morogoro |
Wilaya | Kilosa |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 18,352 |
Rudewa ni jina la kata ya Wilaya ya Kilosa katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67411. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 18,352 waishio humo. [1]
Kilimo cha mpunga na mahindi ni kati ya vitu ambavyo wananchi wanavitegemea pamoja na kiwanda cha mkonge kilichopo Rudewa Kambini.
Ina shule za msingi kama Rudewa Batini, Rudewa Mbuyuni, Rudewa Peapea, Unone na Rudewa Gongoni. Pia ina shule ya sekondari ya Rudewa.
Kata hii ina mabonde na mito isiyokauka kama mto Wami.
Wafugaji pia wanapatikana kama Wamasai na Wasukuma, mbali ya makabila kama Waha, Wamakua, Wamatumbi na Wazigua.
Ina vijiji kama Peapea, Mbuyuni, Rudewa, Gongoni na Unone.
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ http://www.meac.go.tz/sites/default/files/Statistics/Tanzania%20Population%20Census%202012.pdf Archived 3 Machi 2016 at the Wayback Machine. Kilosa - Morogoro
![]() |
Kata za Wilaya ya Kilosa - Mkoa wa Morogoro - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Berega | Chanzulu | Dumila | Kasiki | Kidete | Kidodi | Kilangali | Kimamba A | Kimamba B | Kisanga | Kitete | Lumbiji | Lumuma | Mabula | Mabwerebwere | Madoto | Magole | Magomeni | Magubike | Maguha | Malolo | Mamboya | Masanze | Mbigiri | Mbumi | Mhenda | Mikumi | Mkwatani | Msowero | Mtumbatu | Mvumi | Parakuyo | Ruaha | Rudewa | Ruhembe | Tindiga | Ulaya | Uleling`ombe | Vidunda | Zombo | |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Rudewa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |