Nenda kwa yaliyomo

Rais

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Rais wa chuo kikuu)
Rais wa Tanzania, John Magufuli (Kulia) akiwa na Dr. Salem Al Ismaily wa Oman

Rais (kutoka Kiarabu: رئیس) ni cheo cha mkuu wa nchi katika serikali ya jamhuri, na pengine mkuu wa taasisi fulani ("mwenyekiti").

Rais wa nchi huwa anachaguliwa ama na wananchi wote au na bunge. Katika nchi kadhaa kuna pia mkutano maalumu unaoitishwa kwa uchaguzi wa rais pekee, kama vile Marekani[1] au Ujerumani [2].

Kuna aina mbili za rais kufuatana na katiba za nchi mbalimbali:

Katika muundo wa serikali ya kibunge shughuli za serikali zinasimamiwa na waziri mkuu. Madaraka ya rais katika muundo huo hufanana na madaraka ya mfalme wa kikatiba isipokuwa hayupo kama rais kwa muda wa maisha yake kama mfalme.

Katika nchi chache, yaani Uswisi, San Marino na Uruguay, kazi za rais hazitekelezwi na mtu mmoja bali na kamati ya viongozi kwa ujumla, kama Halmashauri ya Shirikisho ya Uswisi.

Marejeo

  1. Katika Marekani wananchi wanapigia kura wajumbe wa "electoral college" na hao wanamchagua rais wakikutana mara moja tu
  2. Ujerumani mkutano maalumu wa "Bundesversammlung" unafanywa na wabunge wote wa Bundestag na idadi sawa ya wawakilishi wa mabunge ya majimbo wanaokutana pamoja kwa uchaguzi wa rais pekee.