Nyigu-makuyu
Nyigu-makuyu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Ceratosolen capensis juu ya tunda la mkuyu mwangajo (Ficus sur)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Familia 2, nusufamilia 6:
|
Nyigu-makuyu ni nyigu wadogo sana wa nusufamilia 6 katika familia Agaonidae na Pteromalidae za nusuoda Apocrita ya oda Hymenoptera walio na uhusiano na mikuyu. Mabuu hula maua kadhaa, lakini majike huchavusha maua mengine. Mikuyu haiwezi kuzaa bila nyigu hawa. Hata hivyo, spishi fulani (hasa katika nusufamilia zilizoorodheshwa za Pteromalidae) hudanganya kwa kutaga mayai ndani ya kuyu kwa msaada wa neli ndefu sana ya kutagia. Kwa hivyo hawaingii kuyu na kuchavusha maua.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Nyigu-makuyu kwa ujumla ni wadogo sana na majike wa spishi nyingi ni mm 1.5-3 tu bila neli ya kutagia, ingawa baadhi huweza kuwa hadi mm 5. Madume ni wadogo zaidi na wadogo kabisa si zaidi ya mm 0.4. Nyigu-makuyu wa kike wana mabawa yenye vena chache sana, lakini madume wa takriban spishi zote hawana mabawa. Rangi pia hutofautiana, majike wakiwa weusi au kahawia na madume hudhurungi. Majike wa spishi za Pteromalidae mara nyingi huwa na rangi ya kijani au bluu inayong'aa kama metali. Majike hubeba neli ya kutagia ambayo siyo ndefu sana katika spishi zinazochavusha. Walakini, katika spishi zisizochavusha neli ni ndefu sana ili kupenya ukuta wa kuyu na kufikia maua.
Biolojia[1]
[hariri | hariri chanzo]Nyigu-makuyu wamegeuka pamoja na mikuyu wanoyochavusha. Kwa hivyo, kila spishi ya nyigu huchavusha spishi moja ya mkuyu tu. Wanapotoka kwenye kuyu, majike huchukua mbelewele kutoka kwa maua ndani ya kuyu. Kisha hutafuta kuyu jingine katika hatua ya awali ya ukuaji na kuingia ndani kupitia kitobo kinachoitwa ostioli. Akishaingia ndani, hutaga mayai kwenye maua mafupi ya kike na katika mchakato huo huchavusha maua marefu zaidi. Maua ya kiume bado hayajaiva kwa wakati huu. Maua yenye mayai huunda kidutu kidogo, ambacho tishu zake ni chakula cha buu yanayoibuka.
Baada ya wiki kadhaa mabuu huwa mabundo. Hatua ya bundo ya madume ni fupi kuliko ile ya majike. Kwa hivyo wanaibuka mapema. Kisha huvunja vidutu vya majike na kuwatungisha. Kwa hivyo majike yanapoibuka tayari wanakuza mayai yao. Wakati huo huo, madume wametafuna tundu kwenye ukuta wa kuyu ili majike waweze kuondoka. Wakati wa kuondoka, huchukua mbelewele kutoka kwa maua ya kiume ambayo yamekomaa kwa wakati. Majike huruka ili kutafuta makuyu mapya kuanzia mchakato huo tena.
Nyigu-makuyu wasiochavusha hawaingii makuyu kupitia ostioli. Badala yake, wana neli ndefu sana za kutagia zinazoweza kupenya ukuta wa kuyu na kufikia maua ya kike. Kwa ujumla hufika makuyu yanapoiva na nyigu wanaochavusha ambao huenda walikuwepo, tayari wameondoka. Spishi nyingine zisizochavusha zinaweza kushindana na zile zinazochavusha. Kwa hali yoyote, ukuaji wa mabuu na kuibuka na kupandana kwa wapevu ni sawa na yale yaliyoelezwa hapo awali. Majike wanapoondoka makuyu, wanaweza kubeba au kutokubeba mbelewele, lakini hata ikiwa ndivyo, hakuna uchavushaji unaotokea bila shaka.
Spishi za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]
Agaonidae
|
Pteromalidae
|
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Ceratosolen galili
-
Jike la Elisabethiella comptoni
-
Majike ya Elisabethiella comptoni wakiondoka kuyu la Ficus abutilifolia
-
Dume la Elisabethiella comptoni
-
Jike la Seres rotundus
-
Majike ya Seres rotundus wakiondoka kuyu la Ficus abutilifolia