Pili Hussein

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Pili Hussein (amezaliwa tar.) ni mmoja kati ya wanawake shujaa nchini Tanzania aliyeweza kutumia ujasiri wake na kujiunga bila woga wowote katika kundi la wanaume na kufanya nao kazi ya uchimbaji madini [1].

Maisha yake ya awali[hariri | hariri chanzo]

Pili alikulia katika familia kubwa. Baba yake ana wake sita na Pili ni mmoja kati ya watoto 38.

Hakupata elimu, hivyo ikapelekea asiwe na chaguo lingine katika maisha yake na kutokana na kutokuwa na furaha katika ndoa yake, Pili alipofikia umri wa miaka 31 aliondoka kwa mume wake na kuelekea migodi ya Mererani, Arusha[2].

Haikuwa rahisi kwa Pili kujihusisha na uchimbaji wa madini pale Mererani kwa kuwa mwanamke. Kutokana na nia, ujasiri na uthubutu Pili aliamua kujifananisha na mwanaMume na kuamua kuvaa suruali iliyokatwa na kuamua kubadili kabisa jina lake na kujiita Anko Hussein ili ajulikane kama mwanamume na kupata nafasi ya kuwa mmoja kati ya wachimbaji madini.

Pili ni mwanamke mwenye nguvu sana, alikuwa na uwezo wa kwenda chini, ndani ya mgodi zaidi ya mita 60 kwa ajili ya kufuata madini kuliko watu wengine na hii ni kutokana na ujasiri na nguvu nyingi alizokuwa nazo[3].

Maisha ya Pili Mgodini[hariri | hariri chanzo]

Pili aliweza kupigania lugha yake japokuwa ilikuwa mbaya na aliweza kubeba kisu kikubwa kama shujaa wa Wamasai. Katika kipindi chote akiwa huko mgodini hakuna yeyote aliyejua kuwa Pili si mwanamume kwani kila kitu alichokuwa akifanya alifanya kama mwanamume.

Baada ya karibu mwaka, Pili aliona makundi mawili ya mawe ya tanzanite, gramu 1000 na gramu 800 kila moja. Wakati huo maisha yake yalianza kubadilika. Aliamua kununua zana zaidi, aliajiri watu waliofanya kazi chini yake.

Kwa sasa, Pili ana wafanyakazi wapatao 70 wanaofanya kazi kwake, ekari 150 za ardhi, ng'ombe 100 na trekta. Anasomesha watoto 32 kutoka katika familia yake na anatamani kufanya kazi na wanawake wadogo kuwafundisha jinsi ya kufanya biashara katika sekta ya madini.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]