Kipanya-mawe
Kipanya-mawe | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 4:
|
Vipanya-mawe ni wanyama wagugunaji wadogo wa jenasi Petromyscus, jenasi pekee ya nusufamilia Petromyscinae katika familia Nesomyidae. Wanafanana na vipanya, lakini hao ni wanafamilia wa Muridae. Wanatokea Afrika ya Kusini katika maeneo yenye mawe na miamba.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Jenasi hii ni tofauti sana na wagugunaji wengine hivi kwamba imewekwa peke yake katika nusufamilia Petromyscinae. Katika miainisho ya hapo awali kipanya-kinamasi (Delanymys brooksi) pia alikuwa amewekwa katika nusufamilia hiyo, lakini sasa ana nusufamilia yake mwenyewe. Vipanya-mawe hupatikana katika Afrika ya Kusini. Wanyama hao wana mfereji wa umbo la V katika taya la juu chini ya jicho wenye ncha kali. Magego yao ni katikati ya jino la mtindo wa mabuku wahenga wa Ulaya (Cricetidae) na jino la mtindo wa vipanya-miti (Dendromurinae).
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Petromyscus barbouri, Kipanya-mawe wa Barbour (Barbour's rock mouse)
- Petromyscus collinus, Kipanya-mawe Kibete (Pygmy rock mouse)
- Petromyscus monticularis, Kipanya-mawe Milima ( Brukkaros pygmy rock mouse)
- Petromyscus shortridgei, Kipanya-mawe wa Shortridge (Shortridge's rock mouse)