Kipanya-mawe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kipanya-mawe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Familia ya juu: Muroidea (Wanyama kama panya)
Familia: Nesomyidae (Wanyama walio na mnasaba na mabuku)
Nusufamilia: Petromyscinae (Wanyana wanaofanana na vipanya-mawe)
Roberts, 1951
Jenasi: Petromyscus
Thomas, 1915
Ngazi za chini

Spishi 4:

Vipanya-mawe ni wanyama wagugunaji wadogo wa jenasi Petromyscus, jenasi pekee ya nusufamilia Petromyscinae katika familia Nesomyidae. Wanafanana na vipanya, lakini hao ni wanafamilia wa Muridae. Wanatokea Afrika ya Kusini katika maeneo yenye mawe na miamba.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Jenasi hii ni tofauti sana na wagugunaji wengine hivi kwamba imewekwa peke yake katika nusufamilia Petromyscinae. Katika miainisho ya hapo awali kipanya-kinamasi (Delanymys brooksi) pia alikuwa amewekwa katika nusufamilia hiyo, lakini sasa ana nusufamilia yake mwenyewe. Vipanya-mawe hupatikana katika Afrika ya Kusini. Wanyama hao wana mfereji wa umbo la V katika taya la juu chini ya jicho wenye ncha kali. Magego yao ni katikati ya jino la mtindo wa mabuku wahenga wa Ulaya (Cricetidae) na jino la mtindo wa vipanya-miti (Dendromurinae).

Spishi[hariri | hariri chanzo]