Petro wa Cava

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Petro akisujudiwa na mtawala.

Petro wa Cava, O.S.B. (jina la Kiitalia: Pietro Pappacarbone; Salerno, 1038 hivi - Cava de' Tirreni, Salerno, 4 Machi 1123) alikuwa amejiunga na monasteri maarufu ya Cava lakini baadaye alihamia Cluny (1062-1068) akawa askofu wa Policastro (1079).

Hata hivyo alijiuzulu arudie monasteri yake ya kwanza akawa abati wake wa tatu akaiongoza kwa uimara hadi kifo chake, alipofuatwa na Kostabile.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Leo XIII tarehe 21 Desemba 1893.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 4 Machi[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.