Petro Dong
Mandhari
Petro Dong | |
Kazi yake | Mtakatifu |
---|
Petro Dong (1800-1862) alikuwa baba wa nyumbani ambaye alikubali kuteswa kikatili kuliko kukanyaga msalaba. Alipoagizwa achanjwe usoni neno “dini ya uongo” aliandikishwa “dini ya ukweli” akakatwa kichwa kwa hilo chini ya kaisari Tu Duc[1].
Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 3 Juni[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Les Missions Etrangères. Trois siecles et demi d'histoire et d'aventure en Asie Editions Perrin, 2008, ISBN 978-2-262-02571-7
- "St. Andrew Dung-Lac & Martyrs", by Father Robert F. McNamara, Saints Alive and All God's Children Copyright 1980-2010 Rev. Robert F. McNamara and St. Thomas the Apostle Church.
- "Vietnamese Martyr Teaches Quiet Lessons", By Judy Ball, An AmericanCatholic.org Web Site from the Franciscans and St. Anthony Messenger Press.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |