Pauline Philipo Gekul
Mandhari
Pauline Philipo Gekul (amezaliwa 25 Septemba 1978) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama cha Mapinduzi (CCM) akitokea kwa mahasimu wao CHADEMA. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Babati Mjini kwanzia mwaka 2015 – mpaka sasa. Mwaka 2020 alichaguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.[1] [2] [3]
Kufuatia kifo cha Rais Magufuli mnamo mwezi Machi 2021, Rais mpya wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki, Samia Suluhu Hassan alimchagua kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Michezo, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
- ↑ Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Pauline Gekul
- ↑ Maelezo ya Mbunge Pauline Gekul
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |