Otilia wa Alsasya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mt. Otilia huko Avolsheim, Alsace

Otilia wa Alsasya (pia Odilia wa Alsace; 662 hivi - 720 hivi huko Mont Sainte-Odile) alikuwa mwanamke wa ukoo maarufu wa Alsace (leo nchini Ufaransa).

Inasemekana alikataliwa na baba yake kwa sababu ya jinsia yake na ya upofu wake, hivyo alilelewa na wakulima.[1]

Miujiza mbalimbali ilitokea katika maisha yake baada ya kupata ubatizo na kuwezeshwa kuona. Alianzisha monasteri mbili na kuwa abesi wake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Mwaka 1807 Papa Pius VII alithibitisha heshima hiyo.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Desemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Saint Odilia of Alsace. Saints.SQPN.com. Iliwekwa mnamo 2012-07-14.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Sala kwa Mt. Otilia, msimamizi wa macho

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Otilia wa Alsasya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.