Othimari
Mandhari
Othimari, O.S.B. (pia: Othmar, Otmar, Audomar; Uswisi, 689 hivi – kisiwa cha Werd, Uswisi, 759 hivi) alikuwa padri ambaye akawa mmonaki na abati wa monasteri ya Kibenedikto aliyoianzisha pamoja na hospitali ya wakoma kwenye chumba cha Galus.
Kwa kuwa alitetea taasisi hizo dhidi ya makabaila, alipelekwa uhamishoni katika kisiwa cha ziwa la Konstanz alipofariki[1].
Mwaka 864 alitangazwa na askofu Solomon I wa Konstanz kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 16 Novemba[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |