Nenda kwa yaliyomo

Oliver N'Goma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Oliver N'Goma
Amezaliwa (1959-03-23)Machi 23, 1959
Mayumba, Gabon
Amekufa 7 Juni 2010 (umri 51)
Libreville, Gabon
Aina ya muziki Zouk, Soukous, Reggae, Afropop
Kazi yake Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo
Miaka ya kazi 1988 – 2010
Studio Lusafrica BMG


Oliver N'Goma (23 Machi 19597 Juni 2010) alikuwa mpiga gitaa na mwimbaji wa muziki wa Afro-zouk na reggae kutoka nchini Gabon. Alipewa jina la utani la "Noli," alizaliwa mjini Mayumba huko mjini kusini-mwagharibi mwa nchi ya Gabon mnamo mwaka wa 1959. Alifahamika sana kwa kibao chake cha mwaka wa 1989 Bane, ambacho kilivumishwa sana na Radio Africa N.1 na Gilles Obringer.

Maisha na muziki

[hariri | hariri chanzo]

N'Goma alivutiwa kimuziki kwa mara ya kwanza na baba yake, mwalimu na mpiga harmoni. Japokuwa amepata masomo yake ya muziki kwa mara ya kwanza wakati ana umri wa miaka nane, ameanza kutumbuiza mbele ya hadhara baada ya kuhamia mjini Libreville kwa ajili ya masomo. Wakati anachukua darasa la uhasibu, amejiunga na Capo Sound, bendi ya shule, ambapo ndipo alipojifunza namna ya kupiga gitaa. Kundi lilikuwa likipiga dansi rasmi na mipira, wamefunza N'Goma sanaaa ya kutumbuiza kwenye jukwaa.

N'Goma alikuwa mwanafunzi maskini kabisa, aliyejizatiti zaidi kwenye muziki na sinema badala ya masomo. Mapenzi yake ya filamu imemwongoza hadi kufanyakazi na TV ya Gabon, ambayo imesafirisha nchini Ufaransa mnamo 1988 ambapo alijifunza kuwa mtu wa kamera.

Wakati anatumia majira ya baridi huko mjini Paris, amemaliza kazi yake ya muziki alioutunga akiwa Gabon. Ametumia pamoja muziki wake na Manu Lima, mtayarishaji wa rekodi mashuhuri kwa muziki wa Kiafrika. Lima alivutiwa sana na kazi bwana mdogo, na kushikilia mwongozo wa rekodi ya kwanza ya N'Goma iliyokwenda kwa jina la Barre.

Albamu ilifurahia mafanikio ya tabu kwa mara ya kwanza, hadi hapo kituo cha redio cha Kiafrika ilipoanza kupiga nyimbo zake. Jina la wimbo huo ilipata ushindi na mafanikio mengi huko Afrika, Ufaransa, na French West Indies, na ulienda kutamba sana katika maeneo hayo. Umefurahia mafanikio sawa tu na yale ya Mario wa Franco au Yeke Yeke wa Mory Kante. Albamu imepata kuwa moja kati ya albamu zilizouza sana katika albamu za Kiafrika hadi sasa.

N'Goma ametoa albamu ya pili, Adia mnamo Desemba 1995, amefanyakazi tena na Manu Lima. Miaka mitano baadaye, albamu yake ya tatu imetoka Seva. Kompilesheni ya vibao vikali, Best of Oliver N'Goma ilitolewa mnamo mwaka wa 2004.

Kifo chake

[hariri | hariri chanzo]

Oliver N’Goma alikufa kwa tatizo la figo kushindwa kufanyakazi vizuri, ugonjwa ambao alikuwa akipambana nao kwa takriban miaka miwili ya mwisho ya maisha yake, mnamo tar. 7 Juni 2010 kwenye Hospitali ya Omar Bongo huko mjini Libreville, Gabon, N'Goma ameiaga dunia.[1]

  1. Robert Kalumba. "King of Zouk Oliver N’goma passes on", 9 Juni 2010. Retrieved on 2010-06-14. 

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

Hanssen, Bjørn-Erik. "Oliver N'Goma". The Leopard Man's African Music Guide. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-05-03. Iliwekwa mnamo 2006-11-14.

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Oliver N'Goma kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.