Nyanda za juu za Ngorongoro
Nyanda za juu za Ngorongoro (kwa Kiingereza: Ngorongoro Highlands au Crater Highlands) ni eneo lenye miinuko lililopo kwenye bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki katika mikoa ya Arusha na Manyara, kaskazini mwa Tanzania.
Jiolojia
[hariri | hariri chanzo]Nyanda za juu za Ngorongoro zinapatikana katika mgawanyiko ambapo bamba la Afrika linagusana na bamba la Somalia, kukutana kwa mabamba haya mawili husababisha maumbile mapya ya kijiolojia kujitokeza.[1]
Kama ilivyo kawaida, sehemu za mgawanyiko kati ya mabamba ya gandunia, maumbile ya kivolkeno huwepo. Hivyo nyanda hizo zina kasoko nyingi na kaldera za kivolkeno. Magma, hupanda kupitia nyufa zilizotokea na kufika kwenye uso wa ardhi na kuunda umbo la koni. Kaldera huundwa pindi volkeno ikilipuka au kuporomoka ndani yake.[1]
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Yafuatayo hupatikana kwenye nyanda za juu za Ngorongoro:
- Kasoko ya Ela Naibori
- Mlima Gelai
- Mlima Kitumbeine
- Ziwa Eyasi
- Vilima vya Meto
- Mlima Loolmalasin
- Kasoko ya Ngorongoro
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Crater Highlands". NASA Earth Observatory. Iliwekwa mnamo 29 Septemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nyanda za juu za Ngorongoro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |