Hifadhi ya Ngorongoro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ngorongoro)
Jump to navigation Jump to search
Makundi ya wanyamapori katika kasoko.
Ramani ya eneo.
Eneo la Ngorongoro lipo kaskazini mwa Tanzania.
Ndani ya kreta.

Ngorongoro ("Ngorongoro Conservation Area") ni eneo la kasoko kubwa nchini Tanzania, lenye umbali wa takriban kilomita 180 kutoka Arusha; pia ni hifadhi ya taifa inayojulikana kote duniani. Eneo hili ni sehemu ya mbeya.

Kuna jumla ya wanyamapori wakubwa takriban 25,000, wakiwa pamoja na vifaru, viboko, nyumbu, pundamilia, nyati, simba, fisi na chui.

Bidii kubwa zaidi ya kulinda wanyama aina ya vifaru zinahitajika haraka kwa sababu idadi ya wanyama hao inazidi kupungua.

Mabaki ya zamadamu katika Olduvai Gorge yanaonyesha kwamba wanyama hao waliokoma walikuweko tangu miaka milioni 3 iliyopita.

Mwaka 1979 Ngorongoro ilipokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO upande wa uasilia.

Katika sekta ya utalii, ambayo nchi kama nchi huitegemea kwa kiasi fulani, ni muhimu serikali iandae miundombinu, hasa barabara zenye ubora wa hali ya juu, ili zitumike kwa muda mrefu na kuboresha sekta nyingine.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Kwa sababu ya aina mbalimbali za wanyama walioko, kreta ya Ngorongoro inafahamika kama kivutio cha utalii duniani.
Mandhari ya kreta ya Ngorongoro.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Ngorongoro Conservation Area at the UNEP World Conservation Monitoring Centre
  • Deocampo, D.M., 2004. Hydrogeochemistry in the Ngorongoro Crater, Tanzania, and implications for land use in a World Heritage Site. Applied Geochemistry, volume 19, p. 755-767
  • Deocampo, D.M., 2005. Evaporative evolution of surface waters and the role of aqueous CO2 in magnesium silicate precipitation: Lake Eyasi and Ngorongoro Crater, northern Tanzania. South African Journal of Geology, volume 108, p. 493-504.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: