Nenda kwa yaliyomo

Ndege ya kijeshi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ndege aina ya F-16 Fighting Falcon ya Israeli Air Force.
Ndege aina ya Grumman F-14 Tomcat ya Marekani mwaka 1991.

Ndege ya kijeshi ni eropleni inayotumiwa kwa kusudi la kijeshi. Mara nyingi ni ndege ilitengenezwa hasa kwa kusudi hilo, lakini kuna pia ndege zinazoitwa hivi hata kama zinafanana na ndege za kawaida hata zinaweza kubaki bila silaha lakini zilinunuliwa na jeshi la nchi fulani kwa makusudi yao. Ndege iliyokodiwa tu au kukamatwa na jeshi kwa muda haiitwi "ndege ya kijeshi".

Puto na putoanga zilitangulia

[hariri | hariri chanzo]

Vyomboanga (balloon) vya kwanza vilivyotumiwa kijeshi vilikuwa puto katika karne ya 19. Zilitumiwa hasa kwa kusudi la kupeleka watazamaji na wapelelezi juu ya uso wa nchi na kupeleleza malengo kwa mizinga na kama mizinga ililenga vema. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kulikuwa pia na matumizi ya putotanga (zeppelin) kwa kusudi hiyohiyo na pia kwa kubeba mabomu nyuma ya mistari ya mapigano. Ndegeputo za Ujerumani zilitupa mabomu kadhaa juu ya London wakati wa Vita Kuu ya Kwanza.

Ndege za injini

[hariri | hariri chanzo]

Mara baada ya kupatikana kwa ndege za akina Wright mnamo mwaka 1903 wanajeshi waliona faida ya kutumia mitambo hiyo kwa makusudi yao. Walileta uwezo wa kufikia mahali haraka zaidi na kwa uhakika zaidi kuliko puto.

Baada ya kuanza kwa Vita vikuu vya kwanza mwaka 1914 marubani walitumwa angani kwa kupeleleza hali ya maadui. Pale ambako ndege za maadui zilikutana angani marubani walianza kupigana kwa kutumia bastola au bunduki walizokuwa nazo.

Mwaka 1915 Ufaransa ilitangulia kutengeneza ndege ya kwanza yenye bombomu.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.