Nenda kwa yaliyomo

Chomboanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Vyomboanga)
Ndege ya kihistoria aina ya Fairey Swordfish

Chomboanga ni chombo cha usafiri chochote kinachoruka juu ya ardhi katika angahewa ya dunia yetu.[1][2][3][4] Vyombo vinvyopita kimo cha kilomita 100 juu ya ardhi huhesabiwa kati ya vyombo vya angani la nje.

Vyomboanga hupatikana kwa namna mbili:

Zikiwa nyepesi kuliko hewa

[hariri | hariri chanzo]
  • Puto - ni fuko kubwa lenye ganda la kitambaa au plastiki lisilopenya gesi. Hujazwa gesi nyepesi hasa heli kwa kusidi ya kupazwa hewani. Puto kubwa lina nguvu elezi ya kutosha ya kubeba mizigo kama chumba cha abiria kadhaa.
  • Ndegeputo (au purutangi) ni kama puto kubwa linalobeba behewa kwa abiria au mizigo ikisukumwa na injini kama eropleni.
    • Ndegeputo kubwa zaidi zina chumba kikubwa cha gesi chenye fremu imara inayobeba ganda. Mfano wake ni hasa ndegeputo aina ya Zeppelin zilizosafirisha abiria kati ya Ulaya na Brazil au Marekani kabla ya vita kuu ya pili ya dunia. Baadaye zilipitiwa na ndege kubwa. Hadi leo kuna majaribio ya mara kwa mara ya kuzirudisha kwenye usafiri lakini ni chache tu zinazojengwa.
    • Blimp ni puto kubwa bila fremu ianyohitaji shindikizo la ndani lililo kubwa kuliko shindikizo ya angahewa. Kuna takriban blimpi 30-40 za kibiashara duniani.

Zikiwa nzito kuliko hewa

[hariri | hariri chanzo]

Picha za Vyomboanga

[hariri | hariri chanzo]
  1. Flight Before Flying by David Wragg (Author) Publisher: ‎Osprey Publishing; First Edition (2 May 1974)Language: ‎English, Hardcover: ‎192 pages, ISBN-10: ‎0850451655, ISBN-13: ‎978-0850451658
  2. World's Air Fleets Hardcover – 1 May 1969 by David Wragg (Author), Publisher: ‎Littlehampton Book Services Ltd; 2nd edition (1 May 1969), Language: ‎English, Hardcover:176 pages ISBN-10: ‎0711000859, ISBN-13: ‎978-0711000858
  3. World's Air Forces Hardcover – 15 Oct. 1971 by David Wragg (Author), Publisher: ‎Osprey Publishing; First Edition (15 Oct. 1971), Language: ‎English, Hardcover: ‎232 pages, ISBN-10: ‎0850450381, ISBN-13: ‎978-0850450385
  4. Speed in the Air, Hardcover – 5 Sept. 1974 by David Wragg (Author), Publisher: ‎Osprey Publishing; 1st ed edition (5 Sept. 1974), Hardcover: ‎192 pages, ISBN-10: ‎0850451752, ISBN-13: ‎978-0850451757

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]