Mwika Kaskazini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mwika Kaskazini ni kata ya Wilaya ya Moshi Vijijini katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Msimbo wa posta ni 25218.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 19,934 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 21,177 [2] walioishi humo. Wenyeji wa eneo hili ni Wachagga na hupenda sana kunywa mbege.

Kata ya Mwika Kaskazini ina vijiji vitano ambavyo ni: Lole Marera, Maringa, Mrimbo Uuo, Msae Kinyamvuo na Nganyeni. Kila kijini kina shule mbili za msingi. Kwa sasa kata hii ina shule mbili za sekondari ambazo ni Lyakirimu na Mwika Secondary. Vijiji hivyo vimetenganishwa na mito inayotiririka toka mlima Kilimanjaro.

Kata ya Mwika Kaskazini ni maarufu kwa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na mazao ya biashara. Wenyeji wa kata hiyo hulima zaidi ndizi, mahindi, mboga (mnafu, sukuma wiki, chainizi, kabeji, majani ya maboga, mchicha na karoti). Pia wenyeji wanalima kahawa ambayo hujipatia kipato chao kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali kama kusomesha watoto na kujenga nyumba zao. Mwika kuna soko kubwa la biashara ambalo huwa linawakusanya wafanyabiashara toka sehemu mbalimbali za Afrika Mashariki. Hili soko ni maarufu kwa uuzaji wa mazao ya vyakula.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Moshi DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-28.
Kata za Wilaya ya Moshi Vijijini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania

Arusha Chini | Kahe Magharibi | Kahe Mashariki | Kibosho Kati | Kibosho Kirima | Kibosho Magharibi | Kibosho Mashariki | Kibosho Okaoni | Kilema Kaskazini | Kilema Kati | Kilema Kusini | Kimochi | Kindi | Kirua Vunjo Kusini | Kirua Vunjo Magharibi | Kirua Vunjo Mashariki | Mabogini | Makuyuni | Mamba Kaskazini | Mamba Kusini | Marangu Magharibi | Marangu Mashariki | Mbokomu | Mwika Kaskazini | Mwika Kusini | Njia Panda | Old Moshi Magharibi | Old Moshi Mashariki | Uru Kaskazini | Uru Kusini | Uru Mashariki | Uru Shimbwe


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mwika Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.