Marangu Magharibi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Marangu Magharibi ni kata ya Wilaya ya Moshi Vijijini katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,976 [1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 25222

Marangu Magharibi ina vijiji 7 na watu wake walio wengi ni wafanyabiashara na wengine wameajiriwa kwenye sekta za binafsi na serikali kwa ujumla. Hata hivyo, ni moja kati ya sehemu maarufu sana, na eneo lake lina rutuba nyingi kwa kilimo kidogo cha ardhi ya hapo iliopo. Ardhi ya eneo hili limerithishwa kwa mtililiko wa kifamilia (mfumo wa "Kihamba"). Umaskini katika eneo hili bado umeonekana kuwa tatizo kubwa lakini linashughulikiwa ukifananisha na sehemu nyingine za mabonde ya Mlima Kilimanjaro. Kuna mito kadhaa inayomwagikia hapa na vilevile vyanzo vya maji ya chemchem.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Moshi DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-28.
Kata za Wilaya ya Moshi Vijijini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania

Arusha Chini | Kahe Magharibi | Kahe Mashariki | Kibosho Kati | Kibosho Magharibi | Kibosho Mashariki | Kilema Kaskazini | Kilema Kati | Kilema Kusini | Kimochi | Kindi | Kirima | Kirua Vunjo Kusini | Kirua Vunjo Magharibi | Kirua Vunjo Mashariki | Mabogini | Makuyuni | Mamba Kaskazini | Mamba Kusini | Marangu Magharibi | Marangu Mashariki | Mbokomu | Mwika Kaskazini | Mwika Kusini | Njia Panda | Okaoni | Old Moshi Magharibi | Old Moshi Mashariki | Uru Kaskazini | Uru Kusini | Uru Mashariki | Uru Shimbwe


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Marangu Magharibi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.