Mwanahamisi Salim Singano
| Mwanahamisi Salim Singano | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Kazi yake | mwanzilishi na mtendaji |
Mwanahamisi Salim Singano (pia anajulikana kama Mishy Singano[1]) ni mwanamke wa Tanzania, mwanzilishi na mtendaji mkuu wa Mkakati Action na Sasasha Consulting company. Mwanahamisi Salim Singano ni mtalaam wa maendeleo ya kimsimu mwenye uzoefu wa kutosha kwenye masuala ya kijamii na mwenye sera za utetezi wa kampeni za kimaendeleo zaidi ya miaka 10.
Ms Singano anafanya kazi kubwa kwenye shirika la Haki za Utetezi Wanawake, na kampeni dhidi ya Unyanyasaji wa kijinsia, Uwezeshaji wa Wanawake, Haki za umilikishwaji wa Ardhi, Mashamba na Haki za chakula, Utawala, Uongozi, na Haki ya Uzazi wa kijinsia[2].
Kutokana na taaluma yake Singano anafanya kazi kubwa na kuongoza Wigo wa ushirikiano ambao unahusisha Serikali na Taasisi za kiserikali za mkoa, na ngazi za kimataifa, ambazo ni Umoja wa Afrika, Benki ya Maendeleo ya Afrika, United Nations Economic Commission for Africa na UNFCCC. Sekta binafsi, INGO’S, Muunganiko wa mwamvuli wa kikanda wa CSO, Jamii za kiraia, Taasisi za Utafiti wa kitaaluma.[3]
Singano alianzisha Sasasha development consulting company kwa ajili ya kuangalia na kutoa Huduma za Kiufundi katika sekta za kimaendeleo na Mkakati Action ni kwa ajili ya kuangalia Uwezezeshwaji wa Wanawake na watoto maeneo ya mijini na sehemu masikini.[4]
Singano amethibitishwa uwezo wake wa kufanya kazi na watu wengine kuwa ni mkubwa na pia ni mwanamke mwenye uwezo wa uongozi wa asili ambae anaweza kuongoza mitaa, kikanda na kimataifa programu za kuhimiza kazi za Utetezi na kampeni za jamii sanasana Haki za Wanawake.
Singano amefanya kazi na vikundi vya watu tofauti tofouti kutokea sehemu mbalimbali za ulimwengu , Baadhi ya nchi ambazo Ms Singano amesafiri kufanya kazi ya kuwaungana mkono kazi anazofanya ni Marekani, Uingereza, Uholanzi,Ubelgiji, Ufaransa, Mexico, Bolivia, Ufilipino, Indonesia, Tunisia, Ethiopia, Kenya, Afrika Kusini, Senegal.
Kazi anazofanya Ms Singano kwa sasa niː̈̇
- Mshauri wa Sekretariati wa Washirika wa maendeleo ya Elimu,
- Mshauri wa mradi wa jinsia-DFID-14ID,
- Mshauri wa maendeleo kampuni ya SASASHA-GEO,
- Mtendaji Mkuu wa Mkakati Action
- Mkurugenzi wa Bodi ya Maendeleo ya mtandao wa jinsia Tanzania,
- Anaongoza wanachama wa Baraza la Afrika Region Mountain forum-
- Mshirika wa Albertine Rift conservation society
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-08. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-08. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-08. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-08. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
| Makala hii kuhusu wasifu wa Mtanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |