Musalia Mudavadi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mudavadi alitumikia kama Waziri mkuu msaidizi nchini Kenya kuanzia Aprili 2008 mpaka Aprili 2013

Wycliffe Musalia Mudavadi ni mwanasiasa maarufu nchini Kenya. Alizaliwa 12 Septemba 1960 katika Wilaya ya Vihiga. Anajulikana zaidi kwa jina la Musalia Mudavadi.

Mudavadi amekuwa mbunge kwa miaka mingi. Aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1989 baada ya baba yake, Moses Mudavadi, aliyekuwa akishikilia kiti hicho kufariki.

Alikuwa ndiye makamu wa rais wa mwisho kabla Daniel Arap Moi hajaondoka madarakani. Inaaminika kuwa alipewa umakamu wa rais ili kushawishi Waluhya kuiunga mkono KANU. Mpango huu haukufanikiwa.

Katika uchaguzi wa urais nchini Kenya mwaka 2002, Mudavadi alikuwa ni mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta. Pamoja na kuungwa mkono na rais aliyekuwa akimaliza muda wake, Moi, na mtandao mkubwa wa KANU, Kenyatta na Mudavadi walishindwa uchaguzi, Kenyatta hakuchaguliwa kuwa rais na Mudavadi alipoteza kiti cha ubunge wa Sabatia.

Wakati wa upigaji wa kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya Kenya, Mudavadi alikuwa kwenye kambi iliyokuwa ikiipinga katiba hiyo. Katika kambi hii alikuwemo mwanasiasa maarufu Raila Odinga.

Mudavadi yuko kwenye kambi ya watakaogombea urais wa Kenya Desemba 2007.

Tovuti

Crystal personal.svg Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Musalia Mudavadi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.