Mng'ong'o
Mandhari
(Elekezwa kutoka Mungango)
Mng'ong'o (Sclerocarya birrea) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mng'ong'o huko Afrika Kusini
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mng'ong'o (pia mng'ongo, mungango au mmorula; jina la kisayansi: Sclerocarya birrea) ni mti mkubwa wa savana. Matunda yake huitwa mang'ong'o au morula.
Mti huu haukuzwi kwa kawaida wala haukatwi ila huachwa porini kwa ajili ya matunda yake. Nyama ya matunda huliwa na kokwa mbichi zake pia. Matunda yanaweza kuchachuliwa ili kutengeneza pombe na hiyo inaweza kukenekwa ili kupata pombe kali (k.m. Amarula).
Juisi iliyochemshwa hutumika ili kukoleza uji uwe mtamu. Kokwa hupondwa ili kutengeneza keki na biskuti au kuweka supu rojorojo. Kokwa zinatoa mafuta pia yanayotumika kwa kupika na kupakia ngozi.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Maua
-
Majani
-
Gome
-
Morula mbichi mtini
-
Morula mbivu
-
Morula zilizoanguka chini
-
Mbegu, moja inaonyesha kokwa
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mng'ong'o kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |