Mtakatifu Plasido

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Mt. Benedikto akimuagiza Mt. Mauro kwenda kumuokoa Mt. Plasido", mchoro wa Filippo Lippi, O.Carm. (1445 hivi).

Mtakatifu Plasido, O.S.B. (Roma, 515- Messina, 541) alikuwa mmonaki wa Italia, mfuasi wa Benedikto wa Nursia, kama inavyoelezwa na Gregori Mkuu katika kitabu "Majadiliano".

Alitumwa Sicilia kuanzisha monasteri nyingine, na huko inasimuliwa kuwa yeye, ndugu zake watatu na wamonaki 30 walivamiwa na kuuawa na maharamia Wavandali wenye chuki kwa Kanisa Katoliki, lakini habari hiyo haina uthibitisho[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 5 Oktoba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.