Monegunda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Monegunda (alifariki Tours, Ufaransa, 3 Juni 570) alikuwa mwanamke Mkristo ambaye baada ya kuolewa na kuzaa watoto wa kike waliowahi kufariki [1] akawa mkaapweke kwa ruhusa ya mume wake[2].

Kwanza aliishi kwao Chartres, halafu akahamia sehemu za Tours ambako alipata wafuasi hadi ikaanzishwa monasteri[3].

Habari zake zimeandikwa na Gregori wa Tours ambaye alimfahamu.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Julai[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "St. Monegundis of France". www.antiochian.org. Iliwekwa mnamo 2016-07-28. 
  2. "St. Monegundis - Saints & Angels - Catholic Online". Catholic Online. Iliwekwa mnamo 2016-07-28. 
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/60420
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.