Nenda kwa yaliyomo

Milima ya Black Hills

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hifadhi ya Kitaifa ya Badlands.
Black Elk Peak.

Milima ya Black Hills ni safu ndogo ya milima inayopakana na tambarare kuu za Marekani kwenye jimbo la Dakota Kusini.

Jina linatokana na muonekano wa milima hii kwa mbali kuwa myeusi kwa sababu ya misitu minene iliyoko.

Wakazi asilia walikuwa Maindio wa makabila ya Wacheyenne na baadaye Walakota. Kuna sehemu ya milima inayotazamwa kuwa ardhi takatifu ya Walakota.

Mnamo 1868, serikali ya Marekani ilifanya Mkataba wa Fort Laramie na Walakota ambamo iliahidi milima hii haitakuwa kamwe eneo kwa walowezi Wazungu.

Lakini baada ya kugunduliwa kwa dhahabu huko kwenye mwaka 1874 milima ilivamiwa na wachimba dhahabu waliofuatwa na jeshi la Marekani. Serikali iliwalazimisha Walakota kuondoka katika Black Hills na kuhamia hifadhi ndogo za kikabila.

Hadi leo Walakota wanakataa kukubali uvamizi huu wakijaribu kwa kila namna kununua sehemu kutoka kwa walowezi wa leo na kutokubali pesa wanayostahili kupewa katika azimio la Mahakama Kuu iliyoamua wanastahili kupewa kutokana na uvamizi wa karne iliyopita.

Baada ya kwisha kwa uchumi wa madini na ukataji miti, tasnia ya utalii imekua. Mlima Rushmore zilimochongwa sanamu kubwa za marais wanne wa Marekani ni kivutio kimojawapo katika Black Hills.


Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]
  • Zieske, Scott (Spring 1985). "Fly Fishing in the Black Hills ca 1910" (PDF). The American Fly Fisher. 12 (2). Manchester, VT: American Museum of Fly Fishing: 22–25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-09-06. Iliwekwa mnamo 2014-11-19.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Milima ya Black Hills kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.