Miaka ya 1960 Nchini Zimbabwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Matukio ya miaka ya 1960 nchini Zimbabwe yanaanza wakati Zimbabwe bado haijapata uhuru.

1960 hadi 1964[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 9 Mei 1960 mchezaji wa criketi wa Zimbabwe Iain Peter Butchart, alizaliwa katika mji wa Bulawayo.

Matangazo ya Televisheni yalianzishwa mnamo Novemba mwaka huo.

Chama cha Zimbabwe African People's Union (ZAPU) kiliundwa mnamo mnamo 1961 huku Joshua Nkomo akiwa kiongozi wake.

Chama cha Rhodesian Front kilishinda uchaguzi mkuu wa Southern Rhodesia mnamo 14 Desemba 1962. Winston Field akawa ndiye Waziri Mkuu wa Rhodesia.

Chama cha Zimbabwe African National Union (ZANU) kiliundwa mnamo 1963 huku Robert Mugabe akiwa Katibu wake Mkuu. Shirikisho la Rhodesia na Nyasaland lilivunjwa mnamo Dsemba 31, 1963 wakati Zambia na Malawi zikikaribia kupata uhuru. Serikali ilimweka Joshua Nkomo, kiongozi na mwanzilishi wa Zimbabwe African Peoples Union katika kizuilio mnamo 16 Aprili 1964 Northern Rhodesia ilipata uhuru na Southern Rhidesia ikawa eneo la ukoloni la Rhodesia mnamo Oktoba 1964.

1965[hariri | hariri chanzo]

Ian Smith aliitangaza Rhodesia kuwa huru kutoka kwa UK mnamo 11 Novemba 1965. Serikali ya Rhodesia iliunda katiba mpya. Herold Wilson, waziri Mkuu wa Britain aliutangaza uhuru huo usio wa halali na kitendo cha uzushi mnamo 12 Novemba. KItengo cha Usalama wa Umoja wa Mataifa kiliutangaza uhuru huo usio halali mnamo 19 Novemba, huku ukiita Britain kumaliza mzozo huo. Serikali ya Britain ilimtimua Gavana na Direkta wa Hazina ya Rhodesia na ikasimamisha hazina zote za Rhodesia nchini Britain mnamo 3 Desemba. Harold Wilson, Britain iliiwekea Rhodesia Vikwazo vya Kiuchumi, huku Waziri Mkuu wa Britain akiuomba umoja wa Mataifa kusaidia katika kmaliza mzozo huo mnamo 16 Desemba. Britain ilitangaza vikwazo vya Mafuta kuingia Rhodesia mnamo 17 Desemba.

1966 hadi 1967[hariri | hariri chanzo]

Kitengo cha Usalama cha Umoja wa Mataifa kilikubali kuwa Britain ilihitajika kutumia nguvu kuzuia mafuta kuingia Rhodesia kupitia Beira, Mozambique mnamo 10 Aprili 1966. Ian Smith, Waziri Mkuu wa Rhodesia, na Harold Wilson, waziri Mkuu wa Britain walikutana mnamo 2 Desemba 1966 katika HMS Tiger kujadili uwezeekano wa Maelewano. Umoja wa Mataifa ulipigakura kuhusu vikwazo vya lazima, vikiwemo vya Mafuta dhidi ya Rhodesia mnamo 16 Desemba. Zimbabwe African People's Union na chama cha Afrika Kusini African National Congress viliunda muungano mnamo Januari 1967 kwa ukabilianaji wa kijeshi dhidi ya Rhodesia na Afrika Kusini. Cuthbert Alport, Baron Alport na aliyekuwa kamishna wa Shirikisho la Afrika ya Kati alizuru Rhodesia mnamo 14 Juni ili kung;amua kama mzozo huu ungeishwa.

1969 hadi 1969[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1968, YMCA ilifunguliwa na Gonarezhou National Park ikaaxhwa bila ulinzi. Umoja wa Mataifa ulikubalia vikwazo vya lazima dhidi ya Rhodesia kupitia kifungu cha 253 mnamo 29 Mei. Ian Smith, waziri Mkuu wa Rhodesia, na Harold Wilson, waziri mkuu wa Britain, walikutana katika HMS Fearless kwa mazungumzo kutoka 10 Oktoba hadi 13 Oktoba. George Thomson, katibu wa Nchi wa Kaswala ya Jumuia ya Madola na Maurice Foley, katibu mdogo wa Nchi ya Britain walizuru Rhodesia kwa mazungumzo mnamo 2 Novemba, ambayo yaliisha bila matokeo ya muhimu. George Thomson and Maurice Foley walikutana na wanamgambo waliotiwa kizuiziniJoshua Nkomo wa Zimbabwe African People's Union na Ndabaningi Sithole, mwanzilishi wa Zimbabwe African National Union, 7 Novemba.

Mchezaji wa Criketi Ebrahim Essop-Adam alizaliwa mjini Harare mnamo 16 Novemba. Serikali ilipanga kura za maoni kwa katiba mpya na kugeuza ncchi hiyo kuwa taifa mnamo 24 Juni. British Residual Mission mjini Salisbury pamoja na Chiumba la Rhodesia Jijini London zote zilifungwa mnamo 14 Julai 1969.