Nenda kwa yaliyomo

Bundi-panga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mascarenotus)
Bundi-panga
Bundi-panga Kaskazi (Surnia ulula)
Bundi-panga Kaskazi (Surnia ulula)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Strigiformes (Ndege kama bundi)
Familia: Strigidae (Ndege walio na mnasaba na bundi)
Nusufamilia: Surniinae (Ndege walio na mnasaba na bundi-panga)
Jenasi: Mascarenotus Mourer-Chauvire, Bour, Moutout & Ribes, 1994

Ninox Pennant, 1769
Sceloglaux Kaup, 1848
Surnia Duméril, 1805
Uroglaux Mayr, 1937

Spishi: Angalia katiba

Bundi-panga ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali za nusufamilia Surniinae katika familia Strigidae.

Wengi baina ya ndege hawa wana ukubwa wa bundi, lakini wengine ni wadogo zaidi na wengine wakubwa zaidi.

Wana rangi ya kahawia au kijivu na wengi wana miraba kwa kidari kama vipanga (hii na jinsi yao ya kuwinda ni sababu za jina lao). Spishi ndogo hula wadudu hasa, lakini spishi kubwa huwinda wanyama, ndege na watambaazi pia. Huwinda wakati wa jioni, usiku na alfajiri na pengine mchana. Mara nyingi wamfukuza windo lao kama kipanga.

Jike huyataga mayai 2-6 katika shimo ndani ya mti.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za kabla ya historia

[hariri | hariri chanzo]
  • Ninox cf. novaeseelandiae (New Caledonian Boobook, mwisho wa Quaternary) – labda inaishi bado
  • Surnia capeki (Mwanzo wa Pleistocene)
  • Surnia robusta (Mwisho wa Pliocene mpaka mwanzo wa Pleistocene)