Marselino wa Karthago

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Marselino wa Karthago (kwa Kilatini: Flavius Marcellinus; alifariki Karthago, leo nchini Tunisia, 13 Septemba 413) alikuwa Mkristo kutoka Toledo (leo nchini Hispania) aliyefikia cheo cha katibu mkuu wa Dola la Roma Magharibi.

Alikuwa rafiki wa Augustino wa Hippo na Jeromu. Augustino aliandika vitabu kadhaa kwa ajili yake.

Aliuawa kwa kusingiziwa na wafuasi wa Donato Mkuu waliomchukia kwa kuwaunga mkono Wakatoliki.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake na ya wenzake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[1][2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.