Marko wa Yerusalemu
Mandhari
Marko wa Yerusalemu (alifariki 185) alikuwa askofu wa kwanza wa Yerusalemu ambaye kwa asili hakuwa Myahudi[1] kuanzia mwaka 134, wakati ambapo mji huo ulijengwa upya na Waroma baada ya Vita vya tatu vya Kiyahudi kama mji wa Kipagani, hadi kifo chake miaka 51 baadaye. Katika muda huo kwa imani na juhudi zake alikusanya tena jumuia ya Kikristo iliyokuwa imesambaratika kwa hofu ya dhuluma. [2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Oktoba[3][4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |