Maria wa Yesu Ekaristi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mt. Maria wa Yesu Ekaristi.

Maria wa Yesu Ekaristi (kwa Kihispania: María de Jesús Sacramentado; jina la awali: Maria Navidad Venegas de la Torre, Zapotlanejo, Jalisco, 8 Septemba 1868 - Guadalajara, 30 Julai 1959) alikuwa mwanamke Mkristo wa Meksiko aliyeanzisha shirika la Mabinti wa Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 22 Novemba 1992, tena mtakatifu tarehe 21 Mei 2000.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Maisha yake hayakuwa na matukio makuu sana.

Alifiwa mama akiwa bado mtoto mdogo na baba akiwa na umri wa miaka 19.

Akiishi na shangazi yake, Maria Navidad alivutiwa sana na maisha ya kitawa akajiunga kwanza na chama cha Mabinti wa Maria (8 Desemba 1898).

Chini ya kiongozi wa kiroho, mwaka 1905 alishiriki mazoezi ya kiroho huko Guadalajara akajiunga na jumuia ya kike yenye kuhudumia wagonjwa hospitalini, iliyoanzishwa na askofu Atenogene Silva y Alvarez Tostado.

Kutokana na sifa zake nyingi, tarehe 25 Januari 1921 akawa mama mkuu na muda mfupi baadaye alitunga katiba ya shirika lake jipya iliyoidhinishwa na jimbo mwaka 1930. Hapo aliweka nadhiri za daima kwa jina la Maria wa Yesu katika Sakramenti.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.