Maria Mikaela Desmaisieres
Mandhari
Maria Mikaela Desmaisieres (Madrid, Hispania, 1 Januari 1809 – Valencia, 24 Agosti 1865) alikuwa mtawa aliyeanzisha shirika la Masista Waabuduo Wajakazi wa Sakramenti Kuu na wa Upendo.
Kabla ya hapo, akisukumwa na upendo mkubwa na hamu ya kumpatia Mungu watu, aliacha maisha ya fahari ya familia yake akajitoa kikamilifu kuhudumia waliopatwa na kipindupindu na kukomboa makahaba[1].
Hatimaye alihudumia tena wenye kipindupindu nayo ikampata na kumuua.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 7 Juni 1925, halafu mtakatifu tarehe 4 Machi 1934.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Agosti[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |