Maria Fransiska wa Yesu
Mandhari
Maria Fransiska wa Yesu[1] (jina la awali: Anna Maria Rubatto; Carmagnola, Torino, Italia, 14 Februari 1844 – Montevideo, Uruguay, 6 Agosti 1904) alikuwa mwanzilishi wa shirika la Masista Wakapuchini wa Mama Rubatto.
Jumuiya hiyo ilianzia Italia na kufanya kazi hasa Amerika Kusini kati ya wahamiajifukara, alipokwenda mwenyewe walau mara saba hadi alipofariki dunia[2].
Tarehe 10 Oktoba 1993 Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri, halafu tarehe 15 Mei 2022 Papa Fransisko mtakatifu, akiwa mtu wa kwanza wa Uruguay kupewa heshima za namna hiyo[3].
Sikukuu yake ni tarehe 6 Agosti[4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |