Nenda kwa yaliyomo

Pepo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mapepo)
Pepo mchafu akiwa angani kadiri alivyofikiriwa na mchoraji; hata hivyo pepo hawana mwili.

Pepo ni roho wachafu au wabaya wenye nguvu za Kishetani wanaoweza kumshawishi mtu atende mabaya na hata kumwingilia kwa lengo la kumharibia maisha yake kiroho na kimwili.

Katika utamaduni wa jumuiya nyingi za Kiafrika, pepo ni tofauti na mizimu ambayo hutazamwa kama roho za ndugu wa karibu wasio na nia mbaya wakitakiwa kuheshimiwa kwa matendo mbalimbali.

Pepo huweza kufikia hatua ya kumpagaa mtu ili kumwendesha afanye mambo mbalimbali kwa kutojielewa kuliko kwa kulewa sana, kama vile kuropoka, kupiga, kurukaruka, kufanya uasherati n.k.

Katika imani ya Kikristo pepo wanaweza kuwa wengi ndani ya mtu mmoja kwa lengo moja (Math 12:45); pia inaaminika kuwa pepo wanaweza kuondolewa kwa mazinguo na katika madhehebu mbalimbali (katika yale ya Kipentekoste hata hadharani) huwa yanafanywa maombi hayo kwa wenye pepo ili kuwaponya kwa kuwafukuza pepo walio ndani yao.

Pepo wanaosadikiwa ni Wakristo ni tofauti na majini wanaosadikiwa na Waislamu kadiri ya dini ya jadi ya Uarabuni.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.