Majadiliano ya mtumiaji:Janeth J Jonathan

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Mr Accountable (majadiliano) 14:59, 27 Novemba 2009 (UTC)[jibu]

Salaaaam![hariri chanzo]

Salam, Janeth. Ninaona unatoa mchango wa haja. Ni furaha yangu kuona dada yangu kama wewe unaleta ladha hizi. Je, umefikiria kuongeza kitu kama interwiki? Makala nyingi nimeona hujaongeza vitu hivyo! Haya, ukiwa na swali, uliza tu, na utajibiwa!--Muddyb MwanaharakatiLonga 07:20, 30 Novemba 2009 (UTC)[jibu]

Salaam tena hata kutoka kwangu. Nafurahia kuona michango yako hasa kwa sababu wewe kama mgeni unajitahidi kwa jumla kutupa lugha inayoeleweka. Ukiwa kwenye mashindano hatuwezi kusahihisha makala zako kabla ya waamuzi kuziangalia ila tu hakuna ubaya kukupa vidokezo kadhaa:
  1. kuhusu umbo la makala zako nimeona umeweka mara nyingi maandishi kabla ya sentensi ya kwanza, hasa jina / sahihi na kitu kama "|- | Milima ya Mahale ||", wakati mwingine pia kichwa cha pekee. Hii hailingani na utaratibu wa makala. Kila makala inapewa kichwa sanifu na pogramu yenyewe, hakuna makala yenye jina la mtungiaji.
  2. Sentensi ya kwanza ina kawaida yake; neno la kwanza (au: kati ya maneno ya kwanza) ni jina la makala kwa herufi koza (bila kichwa cha pekee! - linganisha Milima ya Mahale inayoanza kinyume). Jina kwa herufi koze haitokei baadaye tena.
  3. Ukiandika juu ya mahali kama hifadhi ni vema kutaja mahali kamili (kwa mfano mkoa, wilaya, umbali na mji fulani na kurejea huko kwa viungo vya ndani.
  4. Jambo muhimu ni Jamii (category) na mwishoni kabisa interwiki (orodha ya makala kuhusu jambo lilelile kwa lugha nyingine). Hapo fuata ushauri wa wikipedia:Mwongozo.
  5. Tafakari tena kuhusu makala ya maana. Haitakiwi kuwa na maandishi marefu.
  6. Usitafsiri majina maalumu, mfano makazi. Hapa kwa sehemu kubwa "makazi" hailingani na maana ya "shelter" uliyotafsiri; pia kama watu au kundi la wanamuziki wanajiita "Shelter" usitafsiri!
  7. Unaandika Kiswahili kizuri. Nashauri uepukane na translate.google. Au tumia muda mwingi kunnyosha lugha. Maana makala ulizoleta kutokana na translate.google zina makosa mengi mno.
Nakutakia mema yote, usishangae kama orodha hii imekuwa ndefu. Umeanza kwa mbio, karibu uendelee! --Kipala (majadiliano) 21:39, 7 Desemba 2009 (UTC)[jibu]

Hongera![hariri chanzo]

Hongera unashika haraka. Nafurahi kuiona. Makala za hifadhi zimeboreka kabisa. Sasa kuhusu jamii ukichungulia ndani ya Jamii:Tanzania utaona Jamii:Hifadhi la Taifa Tanzania. Nadhani unaweza kuitumia. Kuhusu Interwiki unaweza kusoma Wikipedia:Makosa#Kusahau Jamii na interwiki. (Asante kwa makosa yako ya kwanza - yamenisaidia kutunga ukurasa huu). Ukiwa na swali uliza tu kwenye kurasa za majadiliano ya makala ya watu au kwenye Wikipedia:Jumuia. --Kipala (majadiliano) 21:07, 8 Desemba 2009 (UTC)[jibu]


Tafadhari nina maswali lakini sijui kama hapa ndio njia sahihi ya kuulizia maswali yangu maana sioni ukurasa ambao ni wa majadiliano ulio bila maneno?

Kwenye kurasa ya majadiliano tuko huru kusema jinsi tunavyopenda. Ukipenda kuweka maswali yako hapa unaweza kuandika; swali ni kama watu watapita hapa kuiona; kwa hiyo wengine wetu wanaandika swali au tatizo mahali hapa halafu wanaweka habari fupi kwenye kurasa za majadiliano ya wanawikipedai ambao wanaombwa kuchangia (Nakuomba pitia ...(kiungo cha mahali). Unaweza pia kuuliza kwenye ukurasa wa Wikipedia:Jumuia ukiweka kichwa kipya na kuuliza chini yake. Hapa ni wengi zaii wanaopita. Karibu tu! --Kipala (majadiliano) 21:51, 8 Desemba 2009 (UTC)[jibu]


Je niko sahihi ninavyorekebisha makala nilizokwisha kuziandika wakati nipo katika mashindano? Pia kwa upande wa interwiki, je ninaziweka katika "Tazama pia" na nisahihi zinavyoonekana kwa rangi nyekundu.

a) Wakati mashindano yanaendelea unaweza kusahihisha. Mwisho wake wakaguzi wanaangalia matokeo. Inaeleweka ya kwamba wageni wetu wanajifunza kazini.
b) interwiki: tazama mfano wa Hifadhi ya Serengeti, utafute kichwa ndani ya en:wikipedia na chukua kutoka huko, halafun uongeze en:JINA katika mabano mraba.
c) afadhali ukumbuke kuweka sahihi yako hapa baada ya kila mchango / swali. --Kipala (majadiliano) 22:27, 8 Desemba 2009 (UTC)[jibu]


nashukuru nimeelewa kiasi. kwa hiyo ni sahihi kwamba interwiki hazionekani katika makala? Na je inabidi niandike nini chini ya kichwa cha "Tazama Pia"? Au sio lazima kuweka? --Janeth J Jonathan (majadiliano) 22:50, 8 Desemba 2009 (UTC)Janeth J Jonathan[jibu]

Majadiliano:Hifadhi ya Mikumi: Interwiki yako haiwezi kufanya kazi. Ukinakili orodha unakili pamoja na kifupi cha lugha au wikipedia nyingine. Ukiongeza ndani ya mabano mraba "de:" kabla ya "Mikumi-Nationalpark" umeshapata interwiki kwa de:wikipedia. Yote ni: [[de:Mikumi-Nationalpark]] . Hii usiweke chini ya kichwa kwa sababu mara unaiweka inaonekana nje ya makala kando kabisa upande wa kushoto wa dirisha la kompyuta. Kichwa kitabaki bila kitu chini yake, ni bure.
Si lazima kuweka "Tazama pia" - hii tunaweza kutumia kama kuna makala ya karibu sana; kwa mfano makala juu ya "Tembo wa Mikumi" (kama ipo).
Njia ya kuboresha ni pia kuongeza viungo vya ndani; chungulia majina ya miji iliyopo tayari, au majina ya mikoa (yako yote, pia wilaya) yanayotajwa kwenye makala, pia ya mito au milima (kama ipo). Lazima uchungulie kwa sababu jina linalojulikana inaweza kuwa "mlima kilimanjaro" au "kilimanjaro (mlima)" au "kilimanjaro" pekee. --Kipala (majadiliano) 23:03, 8 Desemba 2009 (UTC)[jibu]

Naomba uangalie Majadiliano:Meza --Kipala (majadiliano) 06:21, 9 Desemba 2009 (UTC)[jibu]

Muundo wa makala[hariri chanzo]

Janeth, salam. Nimeona mara kadhaa ukiandika makala moja kwa moja bila kusema ni kitu gani. Kwa mfano makala ya Maporomoko ya Kalambo uliandika moja kwa moja (Maporomoko ya Kalambo yapo karibu na mpaka wa Zambia na Ziwa Tanganyika). Wakati kikawaida makala ni lazima kuanza kusema na... Maporomoko fulani ni... Miimi nikabadilisha na kuweka kitu kama: Maporomoko ya Kalambo ni maporomoko ya maji ambayo yapo karibu na mpaka wa Zambia na Ziwa Tanganyika. Basi dada hizo ndizo taratibu za kamusi elezo. Karibu sana na ukiwa una uliza tu. Nikiwa ninatokea Dar es Salaam, Tanzania, niite Muddyb au,--Muddyb MwanaharakatiLonga 09:10, 17 Desemba 2009 (UTC)[jibu]

Salam, ninashukuru kwa kunikosoa maana nimeweza kujifunza kitu kipya na nitajitahidi kutorudia kosa.

--Janeth J Jonathan (majadiliano) 23:38, 17 Desemba 2009 (UTC)Janeth[jibu]

Haya, dada usijali. Pia, ninajambo moja ninataka kukuomba. Je, unaweza kuisawazisha ile makala yako ya Gauni? Nimeona ukielekezwa na Kipala jinsi ya kufanya makala mazuri (halafu baadaye ukarudia zile makala zako na kuziweka saw), lakini hii ya gauni wapi? Makala ile ni kubwa mno. Kuna uwezekano mkubwa wa kupata pointi za juu iwapo utaisahihisha ile makala, dada yangu. Kingine, unaandika makala za mbegu sana - wakati shindano hili linataka makala zenye angalau vichwa vinne. Si lazima, lakini hali halisi ndiyo hiyo, dada yangu! Salam nyingi kutoka Kiwalani, shindano jema!!!--Muddyb MwanaharakatiLonga 05:45, 18 Desemba 2009 (UTC)[jibu]