Nenda kwa yaliyomo

Magonjwa ya macho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jicho lenye conjunctivitis kutokana na virusi.

Magonjwa ya Macho ni maradhi mbalimbali yanayoweza kuyapata macho, kama vile kisukari cha macho na glakoma (presha ya macho).

Jicho ni kiungo kimojawapo cha mwili kinachomsaidia mwanadamu na pia wanyama kuona vitu mbalimbali katika dunia na hata ulimwengu kwa jumla.

Mnyama yeyote akikosa macho ni adhabu kubwa sana kwa maisha yake ambapo asipokuwa na mwangalizi anaweza kupata adha mbalimbali kama kukosa chakula na inaweza kumpelekea mnyama kufa kwa kukosa chakula kwa sababu haoni.

Magonjwa ya macho yapo ya aina mbalimbali: mengine yanasababishwa na nzi, kama vile trakoma, na mengine yanasababishwa na mionzi ambayo inaweza kuwa ya jua, runinga na hata tarakilishi ambavyo vinasababisha macho kutofanya kazi vizuri kama kuona mbali na kuona karibu na pia kichwa kuuma.

Makengesa katika macho yanasababishwa na kulegea kwa mishipa ya siliari inayoshika lenzi ya jicho.

Magonjwa yote ya macho yanatibika; inategemea hatua ya ugonjwa huo wa macho ulipofikia, kama kuona karibu unaweza kupona kwa kutumia lenzi mbonyeo na kuona mbali unatumia lenzi mbinuko kwenye miwani yako ambapo humsaidia mgonjwa kuona vizuri na kuweza kutofautisha vitu mbalimbali na pia ukihisi kama macho yako yanauma unaweza ukala karoti kwa sababu ina Vitamini A inayoweza kukusaidia ukiwa na ukavu macho.

Magonjwa ya macho yanatibika ukiwahi hospitali kwa matibabu zaidi.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Magonjwa ya macho kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.