Trakoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Trakoma
Mwainisho na taarifa za nje
In-turned eyelid and eyelashes as a result of trachoma
ICD-10 A71.
ICD-9 076
DiseasesDB 29100
MedlinePlus 001486
eMedicine oph/118
MeSH D014141

Trakoma, pia inaitwa chembechembe za konjaktiva, Egyptian ophthalmia,[1] na trakoma ya kuwa kipofu ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na bakteria Klamidia trakomati.[2] Maambukizi husababisha kukwaruza sehemu ya ndani ya vigubiko vya macho. Huu mkwaruzo unaweza kusababisha maumivu ya macho, kuharibika kwa sehemu ya nje au konea ya macho, na labda kuwa kipofu.[2]

Kisababishi[hariri | hariri chanzo]

Bakteria inayosababisha ugonjwa unaweza kusambazwa kwa mgusano wa macho au mapua wa moja kwa moja au usiokuwa wa moja kwa moja na mtu aliyeambukizwa.[2] Mgusano wa macho au mapua usiokuwa wa moja kwa moja unajumuisha kupitia nguo au inzi walioguza mtu aliyeambukizwa.[2] Maambukizi mengi huhitajika kwa zaidi ya miaka mingi kabla ya alama iliyoko kwa kigubiko cha jicho haijakuwa kubwa kwamba kope za macho zinaanza kukwaruza jicho.[2] Watoto husambaza ugonjwa kila mara zaidi ya watu wazima.[2] Mazingira chafu, maeneo yaliyo na watu wengi, na pasipo na maji safi ya kutosha na choo yanachangia usambazaji.[2]

Uzuiaji na Matibabu[hariri | hariri chanzo]

Juhudi za kuzuia ugonjwa unajumuisha uboreshaji wa kupata maji safi na kupunguza idadi ya watu walioambukizwa kupitia matibabu ya antibiotiki.[2] Hii inaweza kujumuisha kutibu, wote mara moja, vikundi vyote vya watu vinavyofahamika kuwa na ugonjwa huu kila mara.[3] Kufua nguo haitoshi kuzuia ugonjwa lakini inaweza kuwa bora na hatua zingine.[4] Aina za matibabu hujumuisha azithromycin ya kunywa au tetracycline ya tropikali.[3] Azithromycin hupendelewa kwa sababu inaweza kutumika kama dozi moja tu ya kunywa.[5] Baada ya mkwaruzo wa kigubiko cha jicho kutokea upasuaji unaweza kuhitajika ili kurekebisha sehemu ya kope za macho na kuzuia kuwa kipofu.[2]

Epidemiologia[hariri | hariri chanzo]

Ulimwenguni, takriban watu milioni 80 wako na maambukizi ya hivi karibuni.[6] Katika maeneo mengine maambukizi yanaweza kuwepo kwa ukubwa wa kati ya asilimia 60–90 ya watoto na mara nyingi huathiri wanawake kuliko wanaume kwa sababu ya kuwa karibu na watoto.[2] Ugonjwa huu ni ksababishi cha ukosefu wa kuona vizuri kwa watu milioni 2.2 ambapo milioni 1.2 ni vipofu kabisa.[2] Hutokea mara nyingi kwa nchi 53 za Afrika, Asia, Amerika Kusini na ya Kati na karibu watu milioni 230 wako hatarini.[2] Inachangia hasara ya dola bilioni 8 ya kiuchumi kila mwaka.[2] Ni ya kikundi cha magonjwa kinachojulikana kama magonjwa ya tropikali yasiyozingatiwa.[6]

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]

<marejeleo />

  1. Swanner, Yann A. Meunier ; with contributions from Michael Hole, TakudzwaShumba&B.J. (2014). Tropical diseases : a practical guide for medical practitioners and students. Oxford: Oxford University Press, USA, 199. ISBN 9780199997909. 
  2. 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 Blinding Trachoma Fact sheet N°382. World Health Organization (November 2013). Iliwekwa mnamo 14 March 2014.
  3. 3.0 3.1 Evans JR1, Solomon AW (March 2011). "Antibiotics for trachoma". Cochrane Database Syst Rev 16 (3): CD001860. doi:10.1002/14651858.CD001860.pub3 . PMID 21412875 .
  4. Ejere, HO; Alhassan, MB; Rabiu, M (Apr 18, 2012). "Face washing promotion for preventing active trachoma.". The Cochrane database of systematic reviews 4: CD003659. doi:10.1002/14651858.CD003659.pub3 . PMID 22513915 .
  5. Mariotti SP (November 2004). "New steps toward eliminating blinding trachoma". N. Engl. J. Med. 351 (19): 2004–7. doi:10.1056/NEJMe048205 . PMID 15525727 . http://content.nejm.org/cgi/pmidlookup?view=short&pmid=15525727&promo=ONFLNS19.
  6. 6.0 6.1 Fenwick, A (Mar 2012). "The global burden of neglected tropical diseases.". Public health 126 (3): 233–6. doi:10.1016/j.puhe.2011.11.015 . PMID 22325616 .