Nyuki : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Masahihisho
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 1 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q3678601 (translate me)
Mstari 123: Mstari 123:
[[pl:Apiformes]]
[[pl:Apiformes]]
[[pt:Abelha]]
[[pt:Abelha]]
[[ro:Albina]]
[[roa-rup:Alghina]]
[[roa-rup:Alghina]]
[[ru:Пчёлы]]
[[ru:Пчёлы]]

Pitio la 17:57, 9 Machi 2013

Nyuki
Nyuki anayekusanya mbelewele
Nyuki anayekusanya mbelewele
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba sana)
Familia: Apidae (Wadudu walio na mnasaba na nyuki)
Ngazi za chini

Nusufamilia 3:

Nyuki ni wadudu wa familia Apidae wenye mabawa manne angavu na mwiba kwenye nyuma ya mwili wao wanaokusanya mbelewele na mbochi ya maua kama chakula chao. Aina inayojulikana hasa ni nyuki-asali Apis mellifera. Kuna spishi zaidi ya 20,000 zinazojumlishwa na biolojia kati ya nyuki lakini ni wale wa jenasi Apis wanaotengeneza asali inayovunwa na wanadamu.

Nyuki-asali mara nyingi wanafugwa lakini wengine wanaishi porini na asali yao inakusanywa kwa kuvunja mzinga wao. Katika Afrika kwa jumla sehemu ya asali bado inatokana na nyuki asali wa porini lakini ufugaji nyuki unapanua.

Mwili wa nyuki

Mwili wa nyuki

Mwili una pande tatu jinsi ilvyo kwa wadudu wote: kichwa mbele, kidari katikati na tumbo nyuma, halafu jozi tatu za miguu na jozi mbili za mabawa.

Mwili huwa na nywele na ina rangi kali za njano-nyeusi kama onyo dhidi ya maadui.

Nyuma ya tumbo wanabeba mwiba wanaotumia kudunga wakijisikia wameshambuliwa. Wakidunga mwiba wanaingiza pia kiasi kidogo cha sumu katika kidonda. Sumu hii inasababisha maumivu na watu wengine wanaathiriwa vikali lakini si kila mtu. Kuna nyuki wanaokufa baada ya kudunga kwa sababu mwiba unabaki kwenye kidonda lakini wengine wanaweza kutoa mwiba na kudunga tena.

Wadudu wa kijamii

Nyuki-asali ni wadudu wa kijamii maana yake wanaishi katika kundi si peke yao kama aina nyingine za nyuki. Wanajenga sega ya nta ndani ya mzinga wa nyuki na humu wanatunza asali yao.

Kuna aina tatu za nyuki ndani ya kundi na mzinga wao ambao ni

  • malkia wa nyuki ni mama wa nyuki wote ndani ya kundi na kazi yake ni kutaga mayai pekee
  • nyuki wafanyakazi ni wakazi wengi wa mzinga na wote ni wa kike. Ni hao wanaofanya kazi yote kama kukusanya mbelewele na mbochi, kusafisha mzinga, kutengeneza nta, kujenga sega, kumlisha malkia na majana, kultetea mzinga
  • nyuki dume ni wachache na kazi yao ya pekee ni kukwea malkia lakini si yule wa mzinga wake kwa kawaida; baadaye wanafukuzwa kwenye mzinga na hawapewi chakula tena

Spishi na nususpishi za Afrika

Spishi za Asia

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyuki kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.