Wagogo : Tofauti kati ya masahihisho
d roboti Badiliko: en:Gogo people |
wikify |
||
Mstari 1: | Mstari 1: | ||
'''Wagogo''' (mmojawao anaitwa Mgogo) ni [[kabila]] la [[Tanzania]] ya kati, wenyeji wa mikoa ya [[Mkoa wa Dodoma|Dodoma]] na [[Mkoa wa Singida|Singida]]. |
'''Wagogo''' (mmojawao anaitwa Mgogo) ni [[kabila]] la [[Tanzania]] ya kati, wenyeji wa mikoa ya [[Mkoa wa Dodoma|Dodoma]] na [[Mkoa wa Singida|Singida]]. [[Lugha]] yao ni [[Cigogo]] (kwa [[Kiswahili]] hutamkika [[Kigogo]]). |
||
⚫ | |||
[[Lugha]] yao ni [[Cigogo]] (kwa [[Kiswahili]] hutamkika [[Kigogo]]). |
|||
== Utawala wa jadi == |
|||
[[Dini]] ya wengi wao ni [[Ukristo]], hasa wa [[madhehebu]] ya [[Anglikana]], halafu wa [[Kanisa Katoliki]]. |
|||
⚫ | |||
== Nyumba za asili == |
|||
⚫ | |||
⚫ | Wagogo wamekuwa wakijenga nyumba ambazo huitwa "'''tembe'''". Tangu zamani kuta za tembe zilijengwa kwa fito (sito kwa lugha yao) zilizosukwa kwa kupisha kuzuia mwanga na maji. Vipande vya kuta vilivyosukwa kwa sito vinaitwa "izizi". Tembe huezekwa kwa udongo ambao hushikiliwa na miti midogomidogo (walo). Walo huwa unashikiliwa na miti mikubwa kidogo (mahapa) na mahapa hushikiliwa na miti mikubwa (Michichi). Michichi ambayo ndiyo hubeba uzito wote hushikiliwa na nguzo kubwa za miti imara na migumu. Nguzo hizo hutiwa masumbiri. Kwa miaka ya karibuni na hata sasa kuta za tembe hujengwa na matofali yanayotengenezwa kwa udongo. |
||
== Chakula kikuu == |
|||
⚫ | |||
⚫ | Wagogo hula [[ugali]] wa [[uwele]] kama chakula kikuu na huchukulia ugali wa [[mahindi]] kama mwepesi. Miaka ya zamani mlo wa kawaida wa Mgogo mwenye uwezo (yaani mwenye [[ng'ombe]]) ulihusisha ugali, [[maziwa]], [[mafuta]] ya ng'ombe, na [[mboga]] kama [[mlenda]], [[safwe]], n.k. Kwa miaka ya sasa Wagogo wamekuwa wakila chakula cha kawaida kama makabila mengine nchini Tanzania. |
||
== Lafudhi ya lugha == |
|||
⚫ | |||
⚫ | kabila la Wagogo lina makabila mengine madogomadogo ndani yake. Wao hutofautiana kwa jinsi ambavyo hutamka maneno au huongeza na kupunguza baadhi ya matamshi kwenye neno. Moja ya makundi yanayoonekana wazi kwenye kabila hili ni kama Wanyambwa ambao huongea lafudhi ya Kinyambwa. Wanyambwa hutokea vijiji vya magharibi mwa [[mji]] wa [[Dodoma]]. Wengine ni Wanyaugogo ambayo huongea lafudhi iitwayo Chinyaugogo. Wanyaugogo ambao ndio wanaowakiLisha kundi kubwa sana hutokea vijiji vya mashariki na kusini mwa mji wa Dodoma na pia [[Mpwapwa]]. |
||
== Majina ya ukoo ya Cigogo == |
|||
⚫ | |||
⚫ | |||
⚫ | |||
⚫ | |||
{{mbegu}} |
{{mbegu}} |
||
Pitio la 01:09, 18 Septemba 2010
Wagogo (mmojawao anaitwa Mgogo) ni kabila la Tanzania ya kati, wenyeji wa mikoa ya Dodoma na Singida. Lugha yao ni Cigogo (kwa Kiswahili hutamkika Kigogo).
Dini ya wengi wao ni Ukristo, hasa wa madhehebu ya Anglikana, halafu wa Kanisa Katoliki. Historia ya Wagogo inaweza kuelezeka kwa kuangalia yafuatayo: Utawala wa jadi, nyumba za asili, chakula kikuu na lafudhi ya lugha.
Utawala wa jadi
Wagogo walikuwa wakiongozwa na mtu mmoja aliyeitwa Mtemi. Watemi kadhaa waliongoza kabila hilo kabla ya mfumo wa uongozi kuvurugwa na ukoloni. Mtemi wa mwisho aliitwa Mazengo ambaye alitokea katika kijiji cha Mvumi, wilaya ya Dodoma vijijini.
Nyumba za asili
Wagogo wamekuwa wakijenga nyumba ambazo huitwa "tembe". Tangu zamani kuta za tembe zilijengwa kwa fito (sito kwa lugha yao) zilizosukwa kwa kupisha kuzuia mwanga na maji. Vipande vya kuta vilivyosukwa kwa sito vinaitwa "izizi". Tembe huezekwa kwa udongo ambao hushikiliwa na miti midogomidogo (walo). Walo huwa unashikiliwa na miti mikubwa kidogo (mahapa) na mahapa hushikiliwa na miti mikubwa (Michichi). Michichi ambayo ndiyo hubeba uzito wote hushikiliwa na nguzo kubwa za miti imara na migumu. Nguzo hizo hutiwa masumbiri. Kwa miaka ya karibuni na hata sasa kuta za tembe hujengwa na matofali yanayotengenezwa kwa udongo.
Chakula kikuu
Wagogo hula ugali wa uwele kama chakula kikuu na huchukulia ugali wa mahindi kama mwepesi. Miaka ya zamani mlo wa kawaida wa Mgogo mwenye uwezo (yaani mwenye ng'ombe) ulihusisha ugali, maziwa, mafuta ya ng'ombe, na mboga kama mlenda, safwe, n.k. Kwa miaka ya sasa Wagogo wamekuwa wakila chakula cha kawaida kama makabila mengine nchini Tanzania.
Lafudhi ya lugha
kabila la Wagogo lina makabila mengine madogomadogo ndani yake. Wao hutofautiana kwa jinsi ambavyo hutamka maneno au huongeza na kupunguza baadhi ya matamshi kwenye neno. Moja ya makundi yanayoonekana wazi kwenye kabila hili ni kama Wanyambwa ambao huongea lafudhi ya Kinyambwa. Wanyambwa hutokea vijiji vya magharibi mwa mji wa Dodoma. Wengine ni Wanyaugogo ambayo huongea lafudhi iitwayo Chinyaugogo. Wanyaugogo ambao ndio wanaowakiLisha kundi kubwa sana hutokea vijiji vya mashariki na kusini mwa mji wa Dodoma na pia Mpwapwa.
Majina ya ukoo ya Cigogo
majina hayo ni kama Mazengo, Cidosa, Cilongani, Malecela, Mwaluko, Mavunde, Ndejembi, Manyesela, Mbogambi, Mdachi, Kapaya,Matonya, Mtunya, Kusila (endeleza)
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |