Mtemi Mirambo : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
kiungo
Mstari 17: Mstari 17:
==Viungo vya nje==
==Viungo vya nje==
*Burnett, Lucy, [http://www.blackpast.org/?q=gah/mirambo-ca-1840-1884 Mirambo (ca.1840--1884)] at [[blackpast.org]]
*Burnett, Lucy, [http://www.blackpast.org/?q=gah/mirambo-ca-1840-1884 Mirambo (ca.1840--1884)] at [[blackpast.org]]
*[http://tesdo-tabora.blogspot.de/2012/02/mjue-mtemi-milambo.html Mjue Mtemi Milambo], kwenye blogu ya Tabora economic and social development organization (TESDO), iliangaliwa Februari 2018

{{mbegu-mtu}}
{{mbegu-mtu}}



Pitio la 12:38, 4 Februari 2018

Mchoro kutoka kitabu cha James William Buels kuhusu "Mashujaa wa Afrika" (1890)

Mtemi Mirambo (1840-1884) alikuwa mfalme wa Wanyamwezi katika magharibi ya Tanzania ya leo.

Jina lake la awali lilikuwa "Mtyela Kasanda", lakini ni maarufu zaidi kamaMirambo (yaani "maiti nyingi").

Mirambo aliwahi kutajirika kama mfanyabiashara ya pembe za ndovu na watumwa kwa njia ya misafara kati ya pwani ya Bahari Hindi na Kongo.

Alitumia sehemu kubwa ya utajiri wake kujenga jeshi la binafsi. Kwa kusudi hilo alinunua bunduki aina ya gobori na kukusanya vijana wengi walioitwa "rugaruga". Rugaruga hao walihofiwa kote. Inasemekana ya kwamba kabla ya mapigano walipewa pombe na bangi kwa kusudi la kuongeza ukatili na kupunguza hofu yao ya kifo.

Kwa kawaida vijana hao walikuwa wanaume walioishi bila ukoo na bila familia kisha kutoroka kwenye hali ya utumwa au kuwa wapagazi wa misafara.[1][2] Mirambo aliwapokea na kuwapa silaha na kwa njia hii alishinda maadui na aliweza kupanua eneo lake hadi kuwa mtemi mkuu wa Wanyamwezi[3][4] kuanzia mwaka 1860 hadi kifo chake mnamo 1884[5].

Alisifiwa na Henry Morton Stanley kama "Napoleon Bonaparte Mwafrika" kutokana na ushujaa wake dhidi ya Waarabu waliomuunga mkono Stanley mwenyewe. Hata hivyo hakufaulu kuteka Tabora kutoka mikononi mwao.

Tanbihi

  1. John Iliffe: A Modern History of Tanganyika. Cambridge University Press, Cambridge 1979, uk. 64
  2. The Cambridge History of Africa, vol. 6
  3. The Nyamwezi aristocracy was appalled when someone who was not royalty took over the religiously ceremonial office of ntemi.
  4. The Cambridge History of Africa, vol. 5
  5. It is possible that he was strangled to death, since an old Nyamwezi custom was to strangle their mtemi when they became unfit to rule.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtemi Mirambo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.