Luigi Guanella

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Luigi Guanella uzeeni.
Sanamu ya Mt. Luigi Guanella, Fratta Polesine, Rovigo.

Luigi Guanella (Fraciscio di Campodolcino, karibu na Como, 19 Desemba 1842 – Como, 24 Oktoba 1915) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki kutoka Italia Kaskazini.

Alianzisha mashirika ya kitawa ya Mabinti wa Mt. Maria wa Maongozi ya Mungu (1890) na Watumishi wa Upendo huko Como (24 Machi 1908), akishirikiana na rafiki zake David Albertario na Giuseppe Toniolo, halafu Chama cha Mt. Yosefu (1914) kwa msaada wa mwanachama wake wa kwanza, Papa Pius X.

Yote hayo yalitokana na huruma yake kubwa kwa maskini, ili kuwatimizia mahitaji yao duniani kote.

Kaulimbiu ya Watumishi wa Upendo ni: In Omnibus CharitasUpendo katika mambo yote.

Guanella alitangazwa mwenye heri na Papa Paulo VI mwaka 1964, halafu mtakatifu na Papa Benedikto XVI tarehe 23 Oktoba 2011.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.