Nenda kwa yaliyomo

Lorenzo de' Medici

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Lorenzo (mnamo 1555-1565).

Lorenzo de' Medici (tamka me-di-chi; 1 Januari 1449 - 8 Aprili 1492) alikuwa mfanyabiashara na mwanasiasa katika mji wa Firenze (kwa Kiingereza: Florence) nchini Italia wakati wa karne ya 15. Aliitwa pia na watu wa mji wake Lorenzo il Magnifico (Lorenzo adhimu)[1]. Lorenzo alizaliwa katika familia ya Medici waliokuwa wafanyabiashara tajiri na babu yake Cosimo de' Medici aliwahi kupanda ngazi kuwa mtawala wa Firenze.

Firenze ilikuwa wakati ule dola-mji na jamhuri ya kujitegema iliyokuwa tajiri kutokana na biashara yake ya kimataifa; ilikuwa kitovu cha kiuchumi ambako benki za kwanza za Ulaya zilipoundwa. Utajiri wa mji uliwezesha taasisi za elimu na kazi ya wasanii wengi, na familia ya Medici ilikuwa kati ya wafadhili mashuhuri zaidi wa elimu na sanaa wakati wa Zama za Mwamko.

Lorenzo alitumia utajiri wake kuwa kiongozi halisi wa siasa ya Firenze ingawa hakuchaguliwa katika ofisi yoyote[2]. Wakati wake viongozi waliochaguliwa katika halmashauri ya serikali ya jamhuri hiyo walimtegemea kifedha na kisiasa. Anajulikana zaidi kwa ufadhili wake wa wasanii mashuhuri kama vile Sandro Botticelli na Michelangelo Buonarroti. Ufadhili huo na ujenzi wa majengo mazuri kama makanisa na majumba ulikuwa sababu ya kumwita "il magnifico" (mwadhimu).

Lorenzo mwenyewe alikuwa pia msanii aliyetunga mashairi. Alizaa watoto 10 na mmojawao aliyeitwa Giovanni akawa Papa Leo X.

  1.  Kent, F.W. (2006). Lorenzo De' Medici and the Art of Magnificence. USA: JHU Press. p. 248. ISBN 0801886279.
  2. Guicciardini, Francesco (1964). History of Italy and History of Florence. New York: Twayne Publishers. p. 8.

Kujisomea

[hariri | hariri chanzo]
  • Miles J. Unger, Magnifico: Maisha ya kipaji na nyakati za vurugu za Lorenzo de Medici (Simon na Schuster 2008), wasifu wa Lorenzo.
  • Christopher Hibbert, Nyumba ya Medici: Kuibuka na Kuanguka kwake (Morrow-Quill, 1980); historia ya jumla ya familia.
  • FW Kent, Lorenzo de- Medici na Sanaa ya Ukubwa (The Johns Hopkins Symposia in Comparative History (The Johns Hopkins University Press, 2004); muhtasari wa uhusiano wa Lorenzo na sanaa.
  • Peter Barenboim, Michoro ya Michelangelo - Ufunguo wa Tafsiri ya Medici Chapel (Moscow, Letny Sad, 2006)  .
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lorenzo de' Medici kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.